Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 10, Sehemu 2 · Art. 168

Kuondolewa kutoka afisini

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Jaji wa mahakama yenye mamlaka ya juu anaweza kuondolewa tu kutoka afisini kwa
misingi ya –
  (a) kushindwa kutekeleza majukumu ya afisi kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa
  kimwili au kiakili;
  (b) kukiuka kanuni za utendakazi zilizowekewa majaji wa Mahakama Makuu kupitia
  Sheria ya Bunge.
  (c) kufilisika;
  (d) kutokuwa na umilisi; au
  (e) utovu wa nidhamu, ama katika utekelezaji wa majukumu ya jaji au vinginevyo.
(2) Hatua ya kumuondoa jaji kwenye wadhifa wake inaweza kuanzishwa na Tume
ya Huduma za Mahakama itakayochukua hatua hiyo kivyake au kwa sababu ya
malalamiko yatakayowasilishwa na mtu yeyote kwa Tume hii.
(3) Malalamiko ya mtu kwa Tume ya Huduma za Mahakama chini ya Ibara ya (2)
yatawasilishwa kwa maandishi, yakionyesha ushahidi wa misingi ya madai ya
kumuondoa jaji.
(4) Tume ya Huduma za Mahakama itaangalia malalamiko hayo na iwapo itaridhika
kwamba ushahidi unaobainika wazi chini ya Ibara ya (1), na itatuma malamamiko
hayo kwa Rais.
(5) Katika muda wa siku kumi na nne baada ya kupokea malalamiko hayo, Rais wa
Taifa atamsimamisha kazi jaji huyo, na kwa kuzingatia ushauri wa Tume ya Huduma
za Mahakama –
  (a) iwapo itakuwa ni Jaji Mkuu, itateua mahakama maalum itakayowahusisha -
  (i) Spika wa Baraza la Kitaifa kama mwenyekiti;
  (ii) majaji watatu wa Mahakama ya Juu kutoka kwa mahakama zenye kutumia
  sheria ya kawaida;
  (iii) wakili mmoja mwenye tajriba ya kazi ya miaka kumi na mitano;
  (iv) watu wengine wawili wenye tajriba kuhusu masuala ya umma; au
  (b) iwapo ni jaji mwingine asiye Jaji Mkuu, atateua mahakama maalum
  itakayohusisha -
  (i) mwenyekiti na wanachama wengine watatu ambao wanahudumu au
  wamewahi kuhudumu kama jaji wa mahakama za mamlaka ya juu, au
  ambao wamehitimu kuteuliwa kuhudumu kwenye wadhifa huo, lakini katika
  kila moja ya hali hizo hawajakuwa, katika miaka mitatu inayotangulia,
  wamekuwa wanachama wa Tume ya Huduma ya Mahakama;
  (ii) wakili mmoja mwenye tajriba ya kazi ya miaka kumi na mitano;
  (iii) watu wengine wawili wenye tajriba kuhusu masuala ya umma.
(6) Licha ya kifungu cha (160) (4), mshahara na marupurupu ya jaji ambaye
anasimamishwa kazi chini ya Ibara ya (5) utapunguzwa kwa nusu hadi wakati
ambapo jaji huyo ataondolewa au kurudishwa kazini.
(7) Mahakama maalum inayobuniwa chini ya Ibara ya (5)-
  (a) itatoa kanuni za kuongoza vikao vyake kwa mujibu wa sheria inayorejelewa
  katika Ibara ya (10); na
  (b) kuchunguza suala hilo kwa haraka, kutoa ripoti ya matokeo na kuwasilisha
  mapendekezo ya kutiliwa maanani kwa Rais.
(8) Jaji ambaye haridhiki na uamuzi wa mahakama maalum chini ya kifungu hiki,
anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu kwa Mahakama ya Juu, rufaa hii itakatwa
kati ya siku kumi baada mahakama maalum kutoa mapendekezo yake.
(9) Rais atatoa maamuzi kwa mujibu wa mapendekezo yaliyotolewa na mahakama
maalum kufikia mwisho wa-
  (a) kuisha kwa muda uliotolewa wa kukata rufaa chini ya Ibara ya (8), iwapo rufaa
  kama hiyo haikukatwa; au
  (b) baada ya kukamilika kwa hatua zote za kesi ya rufaa chini ya Ibara ya (8), iwapo
  rufaa kama hiyo imekatwa na uamuzi wa mwisho unaafikiana na mapendekezo ya
  mahakama hiyo maalum.
(10) Bunge litatunga sheria ya kutoa kanuni za kufuatwa na mahakama maalum
itakayoteuliwa chini ya kifungu cha hiki.
Kwa maneno rahisi
  • Jaji anaweza kuondolewa tu kwa kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi, kukiuka kanuni za maadili, kufilisika, kukosa umahiri, au maovu makubwa.
    Art. 168(1)

    (1) Jaji wa mahakama yenye mamlaka ya juu anaweza kuondolewa tu kutoka afisini kwa misingi ya – (a) kushindwa kutekeleza majukumu ya afisi kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kimwili au kiakili; (b) kukiuka kanuni za utendakazi zilizowekewa majaji wa Mahakama Makuu kupitia Sheria ya Bunge. (c) kufilisika; (d) kutokuwa na umilisi; au (e) utovu wa nidhamu, ama katika utekelezaji wa majukumu ya jaji au vinginevyo.

    Soma kifungu kamili →
  • Uondoaji huanzishwa na Tume ya Huduma za Mahakama, na kamati huchunguza na kutoa mapendekezo ya lazima kwa Rais.
    Art. 168(2)

    (2) Hatua ya kumuondoa jaji kwenye wadhifa wake inaweza kuanzishwa na Tume ya Huduma za Mahakama itakayochukua hatua hiyo kivyake au kwa sababu ya malalamiko yatakayowasilishwa na mtu yeyote kwa Tume hii.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Jaji anaweza kuondolewa kwa sababu kubwa tu, kwa mchakato maalum.
    Art. 168(1)

    (1) Jaji wa mahakama yenye mamlaka ya juu anaweza kuondolewa tu kutoka afisini kwa misingi ya – (a) kushindwa kutekeleza majukumu ya afisi kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kimwili au kiakili; (b) kukiuka kanuni za utendakazi zilizowekewa majaji wa Mahakama Makuu kupitia Sheria ya Bunge. (c) kufilisika; (d) kutokuwa na umilisi; au (e) utovu wa nidhamu, ama katika utekelezaji wa majukumu ya jaji au vinginevyo.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →