Sura 10, Sehemu 4 · Art. 173
Hazina ya Mahakama
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kutabuniwa hazina itakayojulikana kama Hazina ya Mahakama ambayo itaongozwa na Msajili Mkuu. (2) Hazina hiyo itatumika kugharamia usimamizi wa Mahakama na majukumu mengine kama itakavyokuwa muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Mahakama. (3) Kila mwaka wa kifedha, Mkuu wa Masjala ataandaa makadirio ya matumizi ya mwaka utakaofuata, na kuyawasilisha kwa Baraza la Kitaifa ili kuidhinishwa. (4) Yakiidhinishwa na Baraza la Kitaifa, matumizi haya yatagharamiwa na Mfuko wa Jumla na fedha hizo zitalipwa moja kwa moja kwa Hazina ya Mahakama. (5) Sheria ya Bunge itabainisha sheria na njia ya kusimamia Hazina hiyo.
Kwa maneno rahisi
- Kuna Mfuko wa Mahakama unaosimamiwa na Msajili Mkuu wa Mahakama.
Art. 173(1)
(1) Kutabuniwa hazina itakayojulikana kama Hazina ya Mahakama ambayo itaongozwa na Msajili Mkuu.
Soma kifungu kamili → - Mfuko hutumika kwa gharama za uendeshaji wa Mahakama.
Art. 173(2)
(2) Hazina hiyo itatumika kugharamia usimamizi wa Mahakama na majukumu mengine kama itakavyokuwa muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Mahakama.
Soma kifungu kamili → - Msajili Mkuu huandaa makadirio ya matumizi na kuyawasilisha kwa Bunge la Kitaifa kwa idhini.
Art. 173(3)
(3) Kila mwaka wa kifedha, Mkuu wa Masjala ataandaa makadirio ya matumizi ya mwaka utakaofuata, na kuyawasilisha kwa Baraza la Kitaifa ili kuidhinishwa.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Mahakama ina mfuko wake wa kulipia kazi zake.
Art. 173(1)
(1) Kutabuniwa hazina itakayojulikana kama Hazina ya Mahakama ambayo itaongozwa na Msajili Mkuu.
Soma kifungu kamili →