Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 2 · Art. 179

Kamati za mamlaka kuu za Kaunti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mamlaka kuu ya kaunti yamepewa, na yatatekelezwa, na kamati za mamlaka kuu za
Kaunti.
(2) Kamati ya mamlaka kuu ya Kaunti inajumuisha-
  (a) gavana wa kaunti na naibu wake; na
  (b) wanachama walioteuliwa na gavana wa kaunti, kwa idhini ya baraza, kutoka kwa
  watu wasio wanachama wa baraza.
(3) Idadi ya wanachama walioteuliwa kwa mujibu wa ibara ya (2)(b) haitazidi:
  (a) thuluthi moja ya wanachama wa bunge la kaunti kama bunge hilo halina zaidi ya
  wanachama zaidi ya thelathini; au
  (b) kumi; kama baraza lina wanachama thelathini au zaidi.
(4) gavana wa kaunti na naibu wake, watakuwa afisa mkuu na naibu wa afisa mkuu wa
kaunti, mtawalia.
(5) Gavana wa kaunti asipokuwepo, naibu wake ana mamlaka ya kutosha ya kuendesha
shughuli zote na majukumu ya gavana wa kaunti.
(6) Wanachama wa kamati kuu ya kaunti wanawajibikia gavana wa kaunti katika
utekelezaji wa majukumu na mamlaka yao.
(7) Iwapo afisi ya gavana itakuwa wazi, wanachama wa mamlaka kuu ya kaunti
walioteuliwa chini ya ibara ya (2) (b) watakuwa hawana kazi.
Kwa maneno rahisi
  • Mamlaka ya utendaji ya kaunti yanamilikiwa na kutekelezwa na kamati kuu ya kaunti.
    Art. 179(1)

    (1) Mamlaka kuu ya kaunti yamepewa, na yatatekelezwa, na kamati za mamlaka kuu za Kaunti.

    Soma kifungu kamili →
  • Inaundwa na gavana wa kaunti, naibu gavana, na wajumbe walioteuliwa na gavana kwa idhini ya bunge.
    Art. 179(2)

    (2) Kamati ya mamlaka kuu ya Kaunti inajumuisha- (a) gavana wa kaunti na naibu wake; na (b) wanachama walioteuliwa na gavana wa kaunti, kwa idhini ya baraza, kutoka kwa watu wasio wanachama wa baraza.

    Soma kifungu kamili →
  • Gavana wa kaunti akiwa hayupo, naibu gavana hufanya kazi kama gavana.
    Art. 179(5)

    (5) Gavana wa kaunti asipokuwepo, naibu wake ana mamlaka ya kutosha ya kuendesha shughuli zote na majukumu ya gavana wa kaunti.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kamati kuu ya kaunti huendesha kaunti, ikiongozwa na gavana.
    Art. 179(1)

    (1) Mamlaka kuu ya kaunti yamepewa, na yatatekelezwa, na kamati za mamlaka kuu za Kaunti.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →