Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 2 · Art. 180

Uchaguzi wa gavana wa kaunti na naibu wa gavana wa kaunti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Gavana wa kaunti atachaguliwa moja kwa moja na wapiga kura waliosajiliwa katika
kaunti hiyo, siku ile ya uchaguzi mkuu wa wabunge, itakayokuwa Jumanne ya pili
ya mwezi Agosti, baada ya kila miaka mitano.
(2) Kuhitimu kuchaguliwa kuwa gavana wa kaunti, mtu lazima awe amehitimu
kuchaguliwa kuwa mwanachama katika baraza la kaunti.
(3) Ikiwa mgombea kiti cha gavana mmoja tu atateuliwa, mtu huyu atatangazwa kuwa
amechaguliwa.
(4) Ikiwa wagombea kiti cha gavana wawili au zaidi watateuliwa, kura zitapigwa katika
kaunti hiyo na mgombeaji atakayepata kura nyingi zaidi atatangazwa kuwa mshindi.
(5) Kila mgombea kiti cha gavana wa kaunti atamteua mtu mmoja ambaye amehitimu
kuchaguliwa kama gavana wa kaunti kuwa mgombea kiti cha naibu gavana.
(6) Mtu hatahudumu afisini-
  (a) kama gavana wa kaunti kwa vipindi zaidi ya viwili; au
  (b) kama naibu gavana kwa vipindi zaidi ya viwili.
(7) Kwa mujibu wa ibara ya (7), mtu ambaye hajaingia afisi ya gavana wa kaunti
atachukuliwa kuwa amehudumu kwa kipindi kizima, kwa mujibu wa kifungu cha
182 (3) (b).
Kwa maneno rahisi
  • Gavana wa kaunti huchaguliwa moja kwa moja na wapiga kura waliojiandikishwa katika kaunti, Jumanne ya pili ya Agosti kila mwaka wa tano.
    Art. 180(1)

    (1) Gavana wa kaunti atachaguliwa moja kwa moja na wapiga kura waliosajiliwa katika kaunti hiyo, siku ile ya uchaguzi mkuu wa wabunge, itakayokuwa Jumanne ya pili ya mwezi Agosti, baada ya kila miaka mitano.

    Soma kifungu kamili →
  • Kila mgombea wa ugavana humteua mwenzake kama mgombea wa naibu gavana.
    Art. 180(5)

    (5) Kila mgombea kiti cha gavana wa kaunti atamteua mtu mmoja ambaye amehitimu kuchaguliwa kama gavana wa kaunti kuwa mgombea kiti cha naibu gavana.

    Soma kifungu kamili →
  • Mtu hawezi kuwa gavana wa kaunti kwa vipindi zaidi ya viwili.
    Art. 180(7)(a)

    (7) Kwa mujibu wa ibara ya (7), mtu ambaye hajaingia afisi ya gavana wa kaunti atachukuliwa kuwa amehudumu kwa kipindi kizima, kwa mujibu wa kifungu cha 182 (3) (b).

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Wapiga kura huchagua gavana wa kaunti yao kila baada ya miaka mitano, na gavana huhudumu vipindi viwili pekee.
    Art. 180(7)(a)

    (7) Kwa mujibu wa ibara ya (7), mtu ambaye hajaingia afisi ya gavana wa kaunti atachukuliwa kuwa amehudumu kwa kipindi kizima, kwa mujibu wa kifungu cha 182 (3) (b).

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →