Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 2 · Art. 182

Nafasi katika afisi ya gavana wa kaunti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Afisi ya gavana wa kaunti itaachwa wazi iwapo anayeshikilia afisi hiyo-
atafariki;
atajiuzulu kwa kumwandikia spika wa baraza la kaunti;
hafai kwa mujibu wa kifungu cha 180 (2);
atapokea kifungo kwa kosa ambalo adhabu yake ni kufungwa gerezani kwa miezi
isiyopungua kumi na miwili;
ataondolewa afisini kwa mujibu wa katiba hii.,
(2) Iwapo afisi ya gavana wa kaunti itakuwa wazi, naibu gavana atatekeleza majukumu
ya gavana kwa kipindi kilichosalia cha gavana kuhudumu.
(3) Iwapo mtu ataikalia afisi kwa mujibu wa ibara ya (2), kwa minajili ya kifungu cha
180(7), mtu huyo atachukuliwa kuwa-
  (a) amehudumu kipindi kizima cha gavana wa kaunti iwapo, kufikia tarehe mtu
  huyo alipoingia afisi hiyo, zaidi ya miaka miwili na nusu imesalia kabla ya tarehe ya
  uchaguzi mwingine ilivyo kawaida chini ya kifungu cha 180 (1); au
  (b) hajahudumu afisini kama gavana wa kaunti iwapo ni hali nyingine yoyote.
(4) Iwapo nafasi itatokea katika afisi ya gavana wa kaunti na ile ya naibu gavana wa
kaunti au iwapo naibu gavana wa kaunti hawezi kuishikilia kwa muda, spika wa
baraza la kaunti atashikilia afisi hiyo kwa muda.
(5) Iwapo nafasi itatokea katika hali inayotjwa katika ibara ya (4), uchaguzi wa gavana
wa kaunti utafanywa kati ya siku sitini baada ya tarehe ya spika kuanza kushikilia
afisi hiyo.
(6) Mtu atakeyechukua nafasi ya kuhudumu katika afisi ya gavana wa kaunti chini
ya kifungu hiki, ila tu aondolewe afisini kwa mujibu wa Katiba hii, ataendelea
kuhudumu hadi gavana mwingine atakapochaguliwa wakati wa uchaguzi unaofuata
kwa mujibu wa kifungu cha 180 (1).
Kwa maneno rahisi
  • Ofisi ya gavana wa kaunti inakuwa wazi kama mshikiliaji akifa, akijiuzulu, akikosa sifa, akihukumiwa kwa kosa zito, au akiondolewa.
    Art. 182(1)

    (1) Afisi ya gavana wa kaunti itaachwa wazi iwapo anayeshikilia afisi hiyo- atafariki; atajiuzulu kwa kumwandikia spika wa baraza la kaunti; hafai kwa mujibu wa kifungu cha 180 (2); atapokea kifungo kwa kosa ambalo adhabu yake ni kufungwa gerezani kwa miezi isiyopungua kumi na miwili; ataondolewa afisini kwa mujibu wa katiba hii.,

    Soma kifungu kamili →
  • Kama nafasi inatokea, naibu gavana huchukua madaraka kama gavana kwa kipindi kilichosalia.
    Art. 182(2)

    (2) Iwapo afisi ya gavana wa kaunti itakuwa wazi, naibu gavana atatekeleza majukumu ya gavana kwa kipindi kilichosalia cha gavana kuhudumu.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama gavana anaondoka madarakani, naibu gavana anachukua nafasi.
    Art. 182(2)

    (2) Iwapo afisi ya gavana wa kaunti itakuwa wazi, naibu gavana atatekeleza majukumu ya gavana kwa kipindi kilichosalia cha gavana kuhudumu.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →