Sura 11, Sehemu 2 · Art. 185
Mamlaka ya kisheria ya mabaraza ya kaunti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mamlaka ya kutunga sheria ya kaunti yamepatiwa na yatatekelezwa na baraza la kaunti. (2) Baraza la kaunti, linaweza kutunga sheria zozote muhimu, zinazoshughulikia masuala yanayohusiana na, ufanikishaji wa mamlaka na majukumu yake, na utekelezaji wa mamlaka ya serikali ya kaunti kwa mujibu wa Mpangilio wa nne. (3) Baraza la kaunti, likizingatia kanuni ya kugawana mamlaka, lina uwezo wa kusimamia kamati ya mamlaka kuu ya kaunti na idara nyingine za mamlaka katika kaunti. (4) Baraza la kaunti laweza kupokea na kuidhinisha mipango na sera kwa- (a) usimamizi na utumiaji wa rasilmali za kaunti; na (b) kustawisha na kusimamia miundomsingi na idara zao.
Kwa maneno rahisi
- Mamlaka ya kutunga sheria ya kaunti yanamilikiwa na kutekelezwa na bunge la kaunti.
Art. 185(1)
(1) Mamlaka ya kutunga sheria ya kaunti yamepatiwa na yatatekelezwa na baraza la kaunti.
Soma kifungu kamili → - Bunge la kaunti linaweza kutunga sheria zinazohitajika kwa utekelezaji wa majukumu ya serikali ya kaunti.
Art. 185(2)
(2) Baraza la kaunti, linaweza kutunga sheria zozote muhimu, zinazoshughulikia masuala yanayohusiana na, ufanikishaji wa mamlaka na majukumu yake, na utekelezaji wa mamlaka ya serikali ya kaunti kwa mujibu wa Mpangilio wa nne.
Soma kifungu kamili → - Bunge la kaunti husimamia kamati kuu ya kaunti.
Art. 185(3)
(3) Baraza la kaunti, likizingatia kanuni ya kugawana mamlaka, lina uwezo wa kusimamia kamati ya mamlaka kuu ya kaunti na idara nyingine za mamlaka katika kaunti.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Bunge la kaunti hutunga sheria za kaunti na huchunguza mamlaka kuu ya kaunti.
Art. 185(2)
(2) Baraza la kaunti, linaweza kutunga sheria zozote muhimu, zinazoshughulikia masuala yanayohusiana na, ufanikishaji wa mamlaka na majukumu yake, na utekelezaji wa mamlaka ya serikali ya kaunti kwa mujibu wa Mpangilio wa nne.
Soma kifungu kamili →