Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 3 · Art. 186

Mamlaka na Majukumu mahususi ya serikali za kaunti na kitaifa

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1 ) Isipokuwa kama ilivyotajwa katika Katiba hii, mamlaka na majukumu ya Serikali ya
taifa na zile za kaunti, mtawalia,ni kama yalivyoelezwa katika Mpangilio wa Nne
(2) Jukumu linalopatikana katika zaidi ya ngazi moja ya Serikali ni jukumu lililo katika
eneo zaidi ya moja la utawala la ngazi hizo za Serikali.
(3) Jukumu ambalo halijatolewa na Katiba hii au na sheria ya taifa kwa kaunti, ni
jukumu ya Serikali ya taifa.
(4) Kuwa yakini zaidi, bunge litatunga sheria ya Jamhuri katika suala lolote.
Kwa maneno rahisi
  • Majukumu na mamlaka ya serikali ya kitaifa na za kaunti yamewekwa katika Mpangilio wa Nne.
    Art. 186(1)

    (1 ) Isipokuwa kama ilivyotajwa katika Katiba hii, mamlaka na majukumu ya Serikali ya taifa na zile za kaunti, mtawalia,ni kama yalivyoelezwa katika Mpangilio wa Nne (2) Jukumu linalopatikana katika zaidi ya ngazi moja ya Serikali ni jukumu lililo katika eneo zaidi ya moja la utawala la ngazi hizo za Serikali. (3) Jukumu ambalo halijatolewa na Katiba hii au na sheria ya taifa kwa kaunti, ni jukumu ya Serikali ya taifa. (4) Kuwa yakini zaidi, bunge litatunga sheria ya Jamhuri katika suala lolote.

    Soma kifungu kamili →
  • Jukumu au mamlaka ambayo hayajapewa kaunti ni jukumu au mamlaka ya serikali ya kitaifa.
    Art. 186(3)

    (3) Jukumu ambalo halijatolewa na Katiba hii au na sheria ya taifa kwa kaunti, ni jukumu ya Serikali ya taifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Bunge linaweza kutunga sheria kwa Jamhuri kuhusu jambo lolote.
    Art. 186(4)

    (4) Kuwa yakini zaidi, bunge litatunga sheria ya Jamhuri katika suala lolote.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mpangilio wa Nne huorodhesha kile serikali ya kitaifa na kaunti kila mmoja hufanya.

    Tafuta →