Sura 11, Sehemu 3 · Art. 187
Kuhamisha mamlaka na majukumu kati ya viwango vya serikali
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mamlaka au majukumu ya Serikali katika kiwango kimoja yaweza kuhamishwa hadi kiwango kingine cha Serikali kwa makubaliano kati ya Serikali hizo mbili kama- (a) mamlaka au jukumu hilo litapata uzito zaidi likitekelezwa na Serikali hiyo itakayolichukua; na (b) kuhamishwa kwa mamlaka au majukumu kunaafikiana na sheria ambazo zinafungamana na utekelezaji wake. (2) Pale ambapo mamlaka au shughuli imehamishwa kutoka kiwango kimoja cha Serikali hadi kwa Serikali ya kiwango kingine- (a) mipango itafanywa ili kuhakikisha kwamba gharama za utekelezaji wa mamlaka au shughuli hiyo iliyohamishwa imefanikishwa; na (b) uwajibikaji wa kikatiba kwa shughuli au mamlaka utahifadhiwa na serikali iliyopangiwa kulingana na Mpangilio wa Nne.
Kwa maneno rahisi
- Jukumu au mamlaka yanaweza kuhamishwa kati ya ngazi za serikali kwa makubaliano kama yatatekelezwa kwa ufanisi zaidi na serikali inayopokea.
Art. 187(1)
(1) Mamlaka au majukumu ya Serikali katika kiwango kimoja yaweza kuhamishwa hadi kiwango kingine cha Serikali kwa makubaliano kati ya Serikali hizo mbili kama- (a) mamlaka au jukumu hilo litapata uzito zaidi likitekelezwa na Serikali hiyo itakayolichukua; na (b) kuhamishwa kwa mamlaka au majukumu kunaafikiana na sheria ambazo zinafungamana na utekelezaji wake.
Soma kifungu kamili → - Jukumu likihamishwa, mipango lazima ihakikishe rasilimali zinazohitajika zinahamishwa pia.
Art. 187(2)(a)
(a) mipango itafanywa ili kuhakikisha kwamba gharama za utekelezaji wa mamlaka au shughuli hiyo iliyohamishwa imefanikishwa; na
Soma kifungu kamili → - Wajibu wa kikatiba wa jukumu hilo unabaki kwa serikali iliyopewa na Mpangilio wa Nne.
Art. 187(2)(b)
(b) uwajibikaji wa kikatiba kwa shughuli au mamlaka utahifadhiwa na serikali iliyopangiwa kulingana na Mpangilio wa Nne.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Serikali zinaweza kukubaliana kugawana baadhi ya kazi, na fedha zake zinahama pia.
Art. 187(1)
(1) Mamlaka au majukumu ya Serikali katika kiwango kimoja yaweza kuhamishwa hadi kiwango kingine cha Serikali kwa makubaliano kati ya Serikali hizo mbili kama- (a) mamlaka au jukumu hilo litapata uzito zaidi likitekelezwa na Serikali hiyo itakayolichukua; na (b) kuhamishwa kwa mamlaka au majukumu kunaafikiana na sheria ambazo zinafungamana na utekelezaji wake.
Soma kifungu kamili →