Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 5 · Art. 189

Ushirikiano wa Serikali ya kitaifa na za kaunti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Serikali katika viwango vyovyote-
  (a) itaendesha na kutumia mamlaka yake ikiheshimu utekelezaji na heshima za
  taasisi nyinginezo za viwango vingine za Serikali na kuheshimu hadhi ya kikatiba na
  taasisi za serikali katika viwango vingine, na kwa serikali ya kaunti, katika kiwango
  cha kaunti;
  (b) kusaidia, kushirikiana na kushauriana na Serikali katika viwango vyote vifaavyo,
  kutekeleza sheria katika viwango vyote vya Serikali; na
  (c) kushauriana na Serikali katika ngazi tofauti tofauti kwa minajili ya kubadilishana
  mawazo, kusimamia sera na utawala, huku uwezo ukikuzwa.
(2) Serikali katika viwango tofauti na serikali tofauti za kaunti zitashirikiana katika
kutekeleza majukumu na mamlaka yao, kwa lengo hilo, zitaunda muungano wa
kamati na mamlaka.
(3) Katika kutofautiana kokote kule kwa Serikali, Serikali inayohusika itafanya kila
jitihada kutatua mzozo huo ikizingatia taratibu za kisheria kama zilivyo katika sheria
ya taifa.
(4) Sheria ya kitaifa itatoa mwongozo na taratibu za kutatua mizozo kati ya Serikali
kwa mbinu m’badala za kutatua mizozo zikiwemo kushauriana, kupatanisha na
kusuluhisha.
Kwa maneno rahisi
  • Serikali za kila ngazi lazima ziheshimu uadilifu wa ngazi nyingine na kusaidiana, kuunga mkono na kushauriana.
    Art. 189(1)

    (1) Serikali katika viwango vyovyote- (a) itaendesha na kutumia mamlaka yake ikiheshimu utekelezaji na heshima za taasisi nyinginezo za viwango vingine za Serikali na kuheshimu hadhi ya kikatiba na taasisi za serikali katika viwango vingine, na kwa serikali ya kaunti, katika kiwango cha kaunti; (b) kusaidia, kushirikiana na kushauriana na Serikali katika viwango vyote vifaavyo, kutekeleza sheria katika viwango vyote vya Serikali; na (c) kushauriana na Serikali katika ngazi tofauti tofauti kwa minajili ya kubadilishana mawazo, kusimamia sera na utawala, huku uwezo ukikuzwa.

    Soma kifungu kamili →
  • Lazima zifanye kila jitihada inayofaa kutatua migogoro, ikiwemo kwa mazungumzo, upatanishi na usuluhishi.
    Art. 189(3)

    (3) Katika kutofautiana kokote kule kwa Serikali, Serikali inayohusika itafanya kila jitihada kutatua mzozo huo ikizingatia taratibu za kisheria kama zilivyo katika sheria ya taifa.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Serikali ya kitaifa na za kaunti lazima zifanye kazi pamoja na kutatua kutokuelewana kwa amani.

    Tafuta →