Sura 11, Sehemu 5 · Art. 190
Usaidizi kwa serikali za kaunti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Bunge litatunga sheria ili kuhakikisha kwamba serikali za kaunti zimepokea usaidizi wa kutosha kuziwezesha kutekeleza majukumu yao. (2) Serikali za kaunti zitaendesha mifumo ya usimamizi wa fedha inayoafikana na matakwa ya sheria ya kitaifa. (3) Bunge litatunga sheria itakayoruhusu serikali ya kitaifa kuingilia serikali ya kaunti iwapo- (a) imeshindwa kutekeleza majukumu yake; au (b) haiendeshi mfumo wa usimamizi wa fedha unaoambatana na matakwa ya sheria ya kitaifa. (4) Sheria inayotawa katika Ibara ya (3) inaweza, hasa, kuipa mamlaka serikali ya kitaifa- (a) kuchukua hatua mwafaka ili kuhakikisha kuwa majukumu ya serikali ya kaunti yanatekelezwa na mfumo wa usimamizi wa fedha unaendeshwa inavyostahili; na (b) kama pana haja, ichukue jukumu la kutekeleza majukumu hayo. (5) Sheria inayotajwa katika Ibara ya (3)- (a) itahitaji notisi kutolewa kwa serikali ya kaunti kuhusu hatua zozote serikali ya kitaifa inadhamiria kuchukua; (b) itaruhusu serikali ya kitaifa kuchukua hatua zilizo muhimu pekee; (c) itahitaji serikali ya kitaifa, wakati inaingilia kati, ichukue hatua ambazo zitaisaidia serikali ya kaunti kurejelea kikamilifu utekelezaji wa majukumu yake; na (d) kutoa utaratibu utakaowezesha seneti kuhusika vyema ili kumaliza au kutoa suluhu kwa matatizo hayo.
Kwa maneno rahisi
- Bunge lazima lihakikishe serikali za kaunti zina msaada wa kutosha kutekeleza majukumu yao.
Art. 190(1)
(1) Bunge litatunga sheria ili kuhakikisha kwamba serikali za kaunti zimepokea usaidizi wa kutosha kuziwezesha kutekeleza majukumu yao.
Soma kifungu kamili → - Bunge hutoa uingiliaji wa serikali ya kitaifa kama kaunti haiwezi kutekeleza majukumu yake au kusimamia fedha vizuri.
Art. 190(3)
(3) Bunge litatunga sheria itakayoruhusu serikali ya kitaifa kuingilia serikali ya kaunti iwapo- (a) imeshindwa kutekeleza majukumu yake; au (b) haiendeshi mfumo wa usimamizi wa fedha unaoambatana na matakwa ya sheria ya kitaifa.
Soma kifungu kamili → - Serikali ya kitaifa, inapoingilia, lazima ichukue hatua zinazosaidia kaunti kurejesha wajibu kamili.
Art. 190(5)(c)
(c) itahitaji serikali ya kitaifa, wakati inaingilia kati, ichukue hatua ambazo zitaisaidia serikali ya kaunti kurejelea kikamilifu utekelezaji wa majukumu yake; na
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Kama serikali ya kaunti inashindwa, serikali ya kitaifa inaweza kuingilia kuisadia irudi kwenye mstari.
Art. 190(3)
(3) Bunge litatunga sheria itakayoruhusu serikali ya kitaifa kuingilia serikali ya kaunti iwapo- (a) imeshindwa kutekeleza majukumu yake; au (b) haiendeshi mfumo wa usimamizi wa fedha unaoambatana na matakwa ya sheria ya kitaifa.
Soma kifungu kamili →