Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 6 · Art. 192

Kusimamishwa kwa muda kwa serikali ya kaunti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti kwa muda-
  (a) wakati wa dharura inayotokana na mizozo ya ndani au vita; au
  (b) wakati wa hali za kipekee zinazohitaji kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo.
(2) Serikali ya kaunti haitasimamishwa kwa muda kulingana na ibara ya (1) (b) hadi
tume huru ifanye uchunguzi wa mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake, Rais wa taifa
aridhike kwamba mashtaka ni ya haki na seneti imeyaidhinisha.
(3) wakati wa kusimamishwa kwa muda katika kifungu hiki, mipango itafanywa ya
kutekeleza majukumu ya kaunti kulingana na Sheria za Bunge.
(4) Seneti yaweza, wakati wowote, kufutilia mbali kusimamishwa huko kwa muda.
(5) kusimamishwa kwa muda katika kifungu hiki hakuwezi kuwa kwa zaidi ya siku
tisini.
(6) Muda uliotengwa kulingana na Ibara ya (5) unapomalizika uchaguzi wa Serikali
mwafaka ya kaunti utafanyika.
Kwa maneno rahisi
  • Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti katika dharura inayotokana na mzozo wa ndani au vita, au katika mazingira mengine ya kipekee.
    Art. 192(1)

    (1) Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti kwa muda- (a) wakati wa dharura inayotokana na mizozo ya ndani au vita; au (b) wakati wa hali za kipekee zinazohitaji kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo.

    Soma kifungu kamili →
  • Kusimamisha katika mazingira ya kipekee kunahitaji tume huru ya uchunguzi, kuridhika kwa Rais, na idhini ya Seneti.
    Art. 192(2)

    (2) Serikali ya kaunti haitasimamishwa kwa muda kulingana na ibara ya (1) (b) hadi tume huru ifanye uchunguzi wa mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake, Rais wa taifa aridhike kwamba mashtaka ni ya haki na seneti imeyaidhinisha.

    Soma kifungu kamili →
  • Kusimamishwa hakuwezi kuzidi siku 90, kisha uchaguzi hufanyika.
    Art. 192(5)

    (5) kusimamishwa kwa muda katika kifungu hiki hakuwezi kuwa kwa zaidi ya siku tisini.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Serikali ya kaunti inaweza kusimamishwa katika hali mbaya sana tu, na kwa muda mfupi.
    Art. 192(1)

    (1) Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti kwa muda- (a) wakati wa dharura inayotokana na mizozo ya ndani au vita; au (b) wakati wa hali za kipekee zinazohitaji kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →