Sura 11, Sehemu 7 · Art. 196
Kushiriki kwa umma, mamlaka, haki na kinga kwa baraza la kaunti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Baraza la kaunti – (a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na (b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katikacshughuli nyingine za baraza na kamati zake. (2) Baraza la kaunti halitawaacha nje watu, au vyombo vya habari, katika kikao chochote ila katika hali ambapo spika wa bunge ametoa uamuzi na sababu za kutosha za kufanya hivyo. (3) Baraza litatunga sheria itakayoonyesha mamlaka, haki, na kinga ya mabaraza ya kaunti, jamii na wanachama wake.
Kwa maneno rahisi
- Bunge la kaunti lazima lifanye shughuli zake kwa uwazi na kufanya vikao vyake hadharani.
Art. 196(1)(a)
(a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na
Soma kifungu kamili → - Lazima liwezeshe ushiriki wa umma katika shughuli zake za kutunga sheria na nyingine.
Art. 196(1)(b)
(b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katikacshughuli nyingine za baraza na kamati zake.
Soma kifungu kamili → - Haliwezi kuwafukuza umma au vyombo vya habari isipokuwa katika mazingira ya kipekee.
Art. 196(2)
(2) Baraza la kaunti halitawaacha nje watu, au vyombo vya habari, katika kikao chochote ila katika hali ambapo spika wa bunge ametoa uamuzi na sababu za kutosha za kufanya hivyo.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Mabunge ya kaunti hukutana hadharani, na watu wanaweza kushiriki.
Art. 196(1)
(1) Baraza la kaunti – (a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na (b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katikacshughuli nyingine za baraza na kamati zake.
Soma kifungu kamili →