Sura 11, Sehemu 7 · Art. 200
Sheria ya kuhusu Sura hii
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Bunge litatunga sheria katika masuala yote muhimu au ya lazima kuidhinisha utekelazaji wa Sura hii. (2) Hasa, sheria inaweza kubuniwa ili iangazie- (a) usimamizi wa mji mkuu, majiji mengine na miji mingine; (b) kuhamishwa kwa majukumu na mamlaka kutoka kwa kiwango kimoja cha Serikali hadi kingine, pamoja na kuhamisha uwezo wa kutunga sheria kutoka kwa Serikali ya kitaifa hadi Serikali za kaunti; (c) taratibu za uchaguzi ama uteuzi wa watu, na kuwatoa mamlakani katika Serikali za kaunti, pamoja na kuhitimu kwa wapiga kura na wagombeaji wa viti. (d) taratibu za mabaraza na kamati kuu pamoja na uenyekiti, mfululizo wa mikutano, uhudhuriaji na upigaji kura; na (e) kusimamishwa kwa muda kwa mabaraza na kamati kuu.
Kwa maneno rahisi
- Bunge lazima litunge sheria kwa mambo yote yanayohitajika kutekeleza Sura hii.
Art. 200(1)
(1) Bunge litatunga sheria katika masuala yote muhimu au ya lazima kuidhinisha utekelazaji wa Sura hii.
Soma kifungu kamili → - Hii inajumuisha uongozi wa mji mkuu, majiji mengine na maeneo ya miji.
Art. 200(2)(a)
(a) usimamizi wa mji mkuu, majiji mengine na miji mingine;
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Bunge hutungasheria zinazofanya ugatuzi ufanye kazi, ikiwemo kwa majiji.
Art. 200(1)
(1) Bunge litatunga sheria katika masuala yote muhimu au ya lazima kuidhinisha utekelazaji wa Sura hii.
Soma kifungu kamili →