Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12 · Art. 203

Ugavi sawa na sheria nyingine za kifedha

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Vigezo vifuatavyo vitatumiwa kutoa uamuzi kuhusu mgao sawa uliotajwa katika
kifungu cha 202 na katika sheria zote za kitaifa kuhusu serikali za kaunti kama
zilivyotungwa kwa mujibu wa masharti ya sura hii –
  (a) masilahi ya kitaifa;
  (b) kifungu kingine ambacho kinahitajika kwa mujibu wa deni la umma na mahitaji
  mengine ya kitaifa;
  (c) mahitaji ya serikali ya kitaifa yatakayoamuliwa kwa misingi ya kigezo cha
  kutopendelea;
  (d) haja ya kuhakikisha kuwa serikali za kaunti zina uwezo wa kutekeleza majukumu
  zilizopewa;
  (e) uwezo wa kifedha na ufanisi wa serikali za kaunti;
  (f) maendeleo na mahitaji mengine ya serikali za kaunti;
  (g) tofauti za kiuchumi miongoni na kati ya kaunti na sababu ya kutatua matatizo
  hayo;
  (h) haja ya kuchukua hatua kwa mujibu wa maeneo na makundi yaliyotengwa;
  (i) haja ya kuboresha uchumi kwenye kila kaunti na kutoa motisha kwa kila kaunti
  kuboresha uwezo wake wa kuzalisha mapato;
  (j) kutamani mgao wa mapato ulio thabiti na unaoweza kutabirika; na
  (k) haja ya wepesi katika kukabiliana na majanga na mahitaji mengine ya muda
  katika misingi ya kigezo cha kutopendelea.
(2) Kwa kila mwaka wa fedha, mgao unaolingana wa mapato yanayozalishwa na taifa
ambayo yatagawiwa serikali za kaunti hayatapungua asilimia kumi na tano ya
mapato yote ambayo serikali ya kitaifa inayozalisha.
(3) Jumla ya fedha zilizotajwa katika Ibara ya (2) zitapigwa hesabu katika
misingi ya ukaguzi wa juzi zaidi wa hesabu ya mapato yaliyokusanywa, kama
itakavyoidhinishwa na Baraza la Kitaifa.
Kwa maneno rahisi
  • Mgao wa haki huamuliwa kwa kuzingatia maslahi ya kitaifa, deni la umma, mahitaji ya ngazi zote mbili za serikali, na tofauti za kiuchumi.
    Art. 203(1)

    (1) Vigezo vifuatavyo vitatumiwa kutoa uamuzi kuhusu mgao sawa uliotajwa katika kifungu cha 202 na katika sheria zote za kitaifa kuhusu serikali za kaunti kama zilivyotungwa kwa mujibu wa masharti ya sura hii – (a) masilahi ya kitaifa; (b) kifungu kingine ambacho kinahitajika kwa mujibu wa deni la umma na mahitaji mengine ya kitaifa; (c) mahitaji ya serikali ya kitaifa yatakayoamuliwa kwa misingi ya kigezo cha kutopendelea; (d) haja ya kuhakikisha kuwa serikali za kaunti zina uwezo wa kutekeleza majukumu zilizopewa; (e) uwezo wa kifedha na ufanisi wa serikali za kaunti; (f) maendeleo na mahitaji mengine ya serikali za kaunti; (g) tofauti za kiuchumi miongoni na kati ya kaunti na sababu ya kutatua matatizo hayo; (h) haja ya kuchukua hatua kwa mujibu wa maeneo na makundi yaliyotengwa; (i) haja ya kuboresha uchumi kwenye kila kaunti na kutoa motisha kwa kila kaunti kuboresha uwezo wake wa kuzalisha mapato; (j) kutamani mgao wa mapato ulio thabiti na unaoweza kutabirika; na (k) haja ya wepesi katika kukabiliana na majanga na mahitaji mengine ya muda katika misingi ya kigezo cha kutopendelea.

    Soma kifungu kamili →
  • Mgao wa haki unaotolewa kwa serikali za kaunti lazima uwe angalau asilimia 15 ya mapato yote yanayokusanywa na serikali ya kitaifa.
    Art. 203(2)

    (2) Kwa kila mwaka wa fedha, mgao unaolingana wa mapato yanayozalishwa na taifa ambayo yatagawiwa serikali za kaunti hayatapungua asilimia kumi na tano ya mapato yote ambayo serikali ya kitaifa inayozalisha.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kaunti lazima zipate angalau asilimia 15 ya fedha ambazo serikali ya kitaifa hukusanya.
    Art. 203(2)

    (2) Kwa kila mwaka wa fedha, mgao unaolingana wa mapato yanayozalishwa na taifa ambayo yatagawiwa serikali za kaunti hayatapungua asilimia kumi na tano ya mapato yote ambayo serikali ya kitaifa inayozalisha.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →