Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12 · Art. 204

Hazina ya Usawazishaji

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kutaundwa Hazina ya Usawazishaji ambayo itachukua asilimia moja unusu ya
mapato yote yanayozalishwa na serikali ya kitaifa kila mwaka, katika misingi ya
ukaguzi wa hesabu za mapato uliofanywa karibuni zaidi, kama itakavyoidhinishwa
na Baraza la Kitaifa.
(2) Serikali ya kitaifa itatumia hazina ya kusawazisha kutoa huduma za kimsingi zikiwa
ni pamoja na maji, barabara, matibabu na umeme katika maeneo yaliyotengwa hadi
kiwango kitakachoboresha huduma hizo katika maeneo hayo kiwe sawa na kiwango
kilicho maeneo mengine, iwezakanavyo.
(3) Serikali ya kitaifa inaweza kutumiaHazina ya Kusawazisha:-
  (a) iwapo matumizi ya fedha za hazina hiyo yameidhinishwa tu katika Mswada wa
  Matumizi ya Fedha uliopitishwa na Bunge; na
  (b) ama kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja kupitia kwa misaada
  yenye masharti ambayo inahusisha makundi yaliyotengwa .
(4) Tume ya Ugavi wa Mapato itashauriwa na mapendekezo yake kutiliwa maanani
mbele ya Bunge ili kupitisha mswada wa kuidhinisha matumizi ya fedha katika
Hazina ya Usawazishaji.
(5) Fedha zozote ambazo hazitakuwa zimetumiwa katika Hazina ya Usawazishaji,
zitasalia katika hazina hiyo kwa matumizi kwa mujibu wa ibara ya (2) na (3) katika
mwaka wa fedha utakaofuata.
(6) Kifungu hiki kitaisha baada ya miaka ishirini kuanzia tarehe kitakapoanza
kutekelezwa, kutegemea ibara ya (7).
(7) Bunge linaweza kupitisha sheria ya kuondoa utekelezaji wa ibara ya (6) kwa kipindi
cha ziada cha miaka mahususi, kutegemea ibara ya (8).
(8) Kupitisha sheria katika ibara ya (7) lazima kuungwe mkono na zaidi ya nusu ya
wabunge wote wa Baraza la Kitaifa, na zaidi ya nusu ya wajumbe wa serikali za
kaunti katika Seneti.
(9) Fedha hazitaondolewa katika Hazina ya Usawazishaji hadi pale Msimamizi wa
Bajeti atakapoidhinisha kutolewa kwake.
Kwa maneno rahisi
  • Kuna Mfuko wa Usawazishaji ambao asilimia 0.5 ya mapato yote yanayokusanywa na serikali ya kitaifa kila mwaka hulipwa.
    Art. 204(1)

    (1) Kutaundwa Hazina ya Usawazishaji ambayo itachukua asilimia moja unusu ya mapato yote yanayozalishwa na serikali ya kitaifa kila mwaka, katika misingi ya ukaguzi wa hesabu za mapato uliofanywa karibuni zaidi, kama itakavyoidhinishwa na Baraza la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Mfuko hutumika kutoa huduma za msingi kama maji, barabara, vituo vya afya na umeme kwa maeneo yaliyotengwa.
    Art. 204(2)

    (2) Serikali ya kitaifa itatumia hazina ya kusawazisha kutoa huduma za kimsingi zikiwa ni pamoja na maji, barabara, matibabu na umeme katika maeneo yaliyotengwa hadi kiwango kitakachoboresha huduma hizo katika maeneo hayo kiwe sawa na kiwango kilicho maeneo mengine, iwezakanavyo.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mfuko maalum husaidia kuleta huduma za msingi kama maji na barabara kwenye maeneo maskini.
    Art. 204(2)

    (2) Serikali ya kitaifa itatumia hazina ya kusawazisha kutoa huduma za kimsingi zikiwa ni pamoja na maji, barabara, matibabu na umeme katika maeneo yaliyotengwa hadi kiwango kitakachoboresha huduma hizo katika maeneo hayo kiwe sawa na kiwango kilicho maeneo mengine, iwezakanavyo.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →