Sura 12, Sehemu 2 · Art. 207
Hazina za mapato za Serikali za Kaunti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Hazina ya Mapato ya kila serikali ya Kaunti imeundwa. Hazina hii italipwa pesa zote zilizozalishwa au kupokelewa na, au kwa niaba ya serikali ya kaunti, isipokuwa fedha ambazo kwa sababu maalum zimetengwa na Sheria ya Bunge. (2) Fedha zinaweza kutolewa kutoka kwa Hazina ya Mapato ya serikali ya Kaunti kwa ajili :- (a) Kama malipo dhidi ya Hazina ya Mapato ambayo yamekubaliwa na Sheria ya Bunge au sheria za serikali hiyo ya kaunti; au (b) kama ilivyoidhinishwa na sheria ya matumizi ya fedha katika serikali hiyo ya kaunti. (3) Fedha hazitatolewa kwa Hazina ya Mapato mpaka Msimamizi wa Bajeti atakapoidhinisha. (4) Sheria ya Bunge inaweza – (a) kutoa idhini zaidi ya kutoa fedha kutoka kwa Hazina ya Mapato ya Serikali ya Kaunti. (b) kuruhusu serikali za kaunti kuanzisha hazina nyingine za mapato na usimamizi wa hazina kama hizo.
Kwa maneno rahisi
- Kuna Mfuko wa Mapato kwa kila serikali ya kaunti ambao fedha zote zinazokusanywa au kupokelewa na kaunti hulipwa.
Art. 207(1)
(1) Hazina ya Mapato ya kila serikali ya Kaunti imeundwa. Hazina hii italipwa pesa zote zilizozalishwa au kupokelewa na, au kwa niaba ya serikali ya kaunti, isipokuwa fedha ambazo kwa sababu maalum zimetengwa na Sheria ya Bunge.
Soma kifungu kamili → - Fedha zinaweza kutolewa kutoka Mfuko wa Mapato wa kaunti tu kama sheria inaruhusu.
Art. 207(2)
(2) Fedha zinaweza kutolewa kutoka kwa Hazina ya Mapato ya serikali ya Kaunti kwa ajili :- (a) Kama malipo dhidi ya Hazina ya Mapato ambayo yamekubaliwa na Sheria ya Bunge au sheria za serikali hiyo ya kaunti; au (b) kama ilivyoidhinishwa na sheria ya matumizi ya fedha katika serikali hiyo ya kaunti.
Soma kifungu kamili → - Fedha haziwezi kutolewa isipokuwa Mdhibiti wa Bajeti aidhinishe.
Art. 207(3)
(3) Fedha hazitatolewa kwa Hazina ya Mapato mpaka Msimamizi wa Bajeti atakapoidhinisha.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Kila kaunti ina mfuko wake wa fedha inazopokea.
Art. 207(1)
(1) Hazina ya Mapato ya kila serikali ya Kaunti imeundwa. Hazina hii italipwa pesa zote zilizozalishwa au kupokelewa na, au kwa niaba ya serikali ya kaunti, isipokuwa fedha ambazo kwa sababu maalum zimetengwa na Sheria ya Bunge.
Soma kifungu kamili →