Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12, Sehemu 3 · Art. 209

Mamlaka ya Kutoza Kodi na Ushuru

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Ni serikali ya kitaifa pekee ambayo imepewa uwezo wa kutoza-
  (a) kodi ya mapato;
  (b) ushuru wa thamani;
  (c) ushuru wa forodha na kodi nyingine katika bidhaa zinazoingizwa na kuuzwa nje
  ya nchi.; na
  (d) mapato ya ushuru.
(2) Sheria ya Bunge inaweza kuipa mamlaka serikali ya kitaifa kutoza ushuru au kodi
nyingine yoyote, isipokuwa ushuru uliotajwa katika ibara ya (3) (a) na (b).
(3) Serikali ya kaunti inaweza kutoza:-
  (a) ushuru kwa mali;
  (b) kodi za burudani; na
  (c) na kodi nyingine yoyote ambayo imeruhusiwa na Sheria ya Bunge.
(4) Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zinaweza kutoza ushuru wa huduma.
(5) Utozaji ushuru na mamlaka mengine ya kuzalisha mapato ya serikali ya kaunti
hautafanywa kwa njia ambayo inakiuka sera za kiuchumi za kitaifa, shughuli za
kiuchumi zinazotekelezwa ndani ya mipaka ya kaunti au uzungushwaji wa bidhaa
katika nchi nzima, huduma, mtaji au ajira.
Kwa maneno rahisi
  • Ni serikali ya kitaifa pekee inayoweza kutoza kodi ya mapato, VAT, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa.
    Art. 209(1)

    (1) Ni serikali ya kitaifa pekee ambayo imepewa uwezo wa kutoza- (a) kodi ya mapato; (b) ushuru wa thamani; (c) ushuru wa forodha na kodi nyingine katika bidhaa zinazoingizwa na kuuzwa nje ya nchi.; na (d) mapato ya ushuru.

    Soma kifungu kamili →
  • Kaunti inaweza kutoza ada za mali, kodi za burudani na kodi nyingine yoyote inayoruhusiwa na Sheria ya Bunge.
    Art. 209(3)

    (3) Serikali ya kaunti inaweza kutoza:- (a) ushuru kwa mali; (b) kodi za burudani; na (c) na kodi nyingine yoyote ambayo imeruhusiwa na Sheria ya Bunge.

    Soma kifungu kamili →
  • Serikali ya kitaifa na za kaunti zinaweza kutoza ada kwa huduma.
    Art. 209(4)

    (4) Serikali ya kitaifa na serikali za kaunti zinaweza kutoza ushuru wa huduma.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Serikali ya kitaifa hukusanya kodi ya mapato na VAT; kaunti hukusanya ada za mali na kodi za burudani.
    Art. 209(1)

    (1) Ni serikali ya kitaifa pekee ambayo imepewa uwezo wa kutoza- (a) kodi ya mapato; (b) ushuru wa thamani; (c) ushuru wa forodha na kodi nyingine katika bidhaa zinazoingizwa na kuuzwa nje ya nchi.; na (d) mapato ya ushuru.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →