Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12, Sehemu 3 · Art. 210

Kutoza Ushuru

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Hakuna kodi yoyote au malipo ya leseni yanayoweza kuondolewa au kubadilishwa
ila kwa mujibu wa sheria.
(2) Iwapo sheria itaruhusu kufutiliwa mbali kwa ushuru au malipo ya leseni –
  (a) rekodi ya kufutilia mbali itahifadhiwa kwa umma ambayo itaonyesha sababu za
  kila kufutilia mbali; na
  (b) kila kufutiliwa mbali; pamoja na sababu zake lazima zifikishwe kwa Mkaguzi
  Mkuu wa Mahesabu.
(3) Hakuna sheria ambayo itamwondolea au kuamrisha mhudumu yeyote wa umma
kutolipa kodi kwa sababu za –
  (a) mamlaka yanayoshikiliwa na afisa huyo; au
  (b) aina ya kazi anayofanya afisa huyo.
Kwa maneno rahisi
  • Hakuna kodi au ada ya leseni inayoweza kutozwa, kuachiliwa au kubadilishwa isipokuwa kama sheria inavyotoa.
    Art. 210(1)

    (1) Hakuna kodi yoyote au malipo ya leseni yanayoweza kuondolewa au kubadilishwa ila kwa mujibu wa sheria.

    Soma kifungu kamili →
  • Hakuna sheria inayoweza kumwondoa afisa wa Serikali kutoka kulipa kodi kwa sababu ya ofisi yake au aina ya kazi yake.
    Art. 210(3)

    (3) Hakuna sheria ambayo itamwondolea au kuamrisha mhudumu yeyote wa umma kutolipa kodi kwa sababu za – (a) mamlaka yanayoshikiliwa na afisa huyo; au (b) aina ya kazi anayofanya afisa huyo.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kodi zinaweza kuundwa au kubadilishwa kwa sheria pekee, na viongozi lazima walipe kodi kama kila mtu.
    Art. 210(1)

    (1) Hakuna kodi yoyote au malipo ya leseni yanayoweza kuondolewa au kubadilishwa ila kwa mujibu wa sheria.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →