Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12, Sehemu 4 · Art. 217

Mgao Unaolingana wa Mapato

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mara moja baada ya kila miaka mitano, Baraza la Seneti litatoa mapendekezo
kuhusu misingi ya kutumiwa katika ugavi wa mapato ya kitaifa yanayogawiwa kila
serikali ya kaunti kila mwaka.
(2) Katika kutoa mapendekezo ya vigezo vya kutumiwa kugawa mapato yaliyotajwa
katika ibara ya (1),Seneti:-
  (a) itatilia maanani kigezo katika kifungu cha 203 (1);
  (b) itaitisha na kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Ugavi wa Mapato;
  (c) itawashauri Magavana wa serikali za kaunti, Waziri anayesimamia fedha na asasi
  nyingine yoyote ya serikali ya kaunti; na
  (d) itawaalika watu, ikiwa ni pamoja na makundi ya wataalamu, kutoa mapendekezo
  yao.
(3) Katika kipindi cha kati ya siku kumi baada ya Seneti kuidhinisha pendekezo chini ya
ibara ya (1), Spika wa Seneti atawasilisha pendekezo hilo kwa Spika wa Baraza la
Kitaifa.
(4) Katika kipindi cha kati ya siku sitini baada ya maamuzi ya Seneti kuwasilishwa
kama inavyotajwa katika ibara ya (3), Baraza la Kitaifa litachunguza pendekezo hilo
na kulipigia kura ili kuliidhinisha kwa kulifanyia au kutolifanyia marekebisho, au
kulikataa.
(5) kiwa Baraza la Kitaifa:-
  (a) halitapiga kura kwa pendekezo hili kwa kipindi cha siku sitini, basi itachukuliwa
  kwamba pendekezo hili limeidhinishwa na Baraza la Kitaifa bila marekebisho;
  (b) litapiga kura kwa pendekezo hili, pendekezo litakuwa:-
  (c) limefanyiwa marekebisho iwapo wajumbe wasiopungua thuluthi mbili wataunga
  mkono marekebisho;
  (i) litakatiliwa iwapo tu wajumbe wa bunge wasiopungua thuluthi mbili
  watalipigia kura ya kulikataa, bila kujali kama limefanyiwa marekebisho na
  Baraza la Kitaifa au la; au
  (ii) kuidhinishwa, kwa njia yoyote ile.
(6) Iwapo Baraza la Kitaifa litaidhinisha pendekezo lililofanyiwa marekebisho au
kulikataa pendekezo, basi Seneti itakuwa na uchaguzi wa:-
  (a) kuchukua pendekezo jipya chini ya ibara ya (1), katika hali hii masharti ya ibara
  ya (4) na (5) yatatumiwa upya;
  (b) kuomba suala hili liwasilishwe kwa kamati ya pamoja ya mabaraza yote mawili
  ya Bunge kwa upatanisho chini ya kifungu cha 113, utakaozingatia marekebisho
  muhimu.
(7) Pendekezo hili chini ya kifungu hiki kitakachokuwa kimeidhinishwa chini ya
ibara ya (5) basi kitaendelea kutekelezwa hadi wakati ambapo pendekezo jipya
litakapoidhinishwa.
(8) Licha ya ibara ya (1), Seneti, kwa uamuzi ikiwa umeungwa mkono na wanachama
wasiopungua thuluthi tatu, inaweza kulifanyia marekebisho pendekezo
lililoidhinishwa.
(9) ibara ya (2) hadi (8), na marekebisho muhimu, zinataja pendekezo chini ya ibara ya
(8).
Kwa maneno rahisi
  • Mara moja kila miaka mitano, Seneti huamua msingi wa kugawa kati ya kaunti sehemu ya mapato ya kitaifa yanayotolewa kwa ngazi ya kaunti.
    Art. 217(1)

    (1) Mara moja baada ya kila miaka mitano, Baraza la Seneti litatoa mapendekezo kuhusu misingi ya kutumiwa katika ugavi wa mapato ya kitaifa yanayogawiwa kila serikali ya kaunti kila mwaka.

    Soma kifungu kamili →
  • Seneti huzingatia vigezo vya Kifungu cha 203(1), mapendekezo ya Tume ya Mgawanyo wa Mapato, na maoni ya umma.
    Art. 217(2)

    (2) Katika kutoa mapendekezo ya vigezo vya kutumiwa kugawa mapato yaliyotajwa katika ibara ya (1),Seneti:- (a) itatilia maanani kigezo katika kifungu cha 203 (1); (b) itaitisha na kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Ugavi wa Mapato; (c) itawashauri Magavana wa serikali za kaunti, Waziri anayesimamia fedha na asasi nyingine yoyote ya serikali ya kaunti; na (d) itawaalika watu, ikiwa ni pamoja na makundi ya wataalamu, kutoa mapendekezo yao.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kila baada ya miaka mitano, Seneti huamua jinsi fedha za kitaifa zinagawanywa kati ya kaunti.
    Art. 217(1)

    (1) Mara moja baada ya kila miaka mitano, Baraza la Seneti litatoa mapendekezo kuhusu misingi ya kutumiwa katika ugavi wa mapato ya kitaifa yanayogawiwa kila serikali ya kaunti kila mwaka.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →