Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12, Sehemu 5 · Art. 221

Mswada wa Makadirio ya Bajeti na Matumizi ya Mwaka

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kwa kipindi kisichopungua miezi miwili kabla ya kukamilika kwa kila mwaka wa
kifedha, waziri anayehusika na fedha, atawasilisha makadirio ya mapato na matumizi
ya mwaka ufuatao wa fedha kwa Baraza la Kitaifa.
(2) Makadirio yaliyotajwa katika ibara ya (1) –
  (a) yatajumlisha makadirio ya matumizi kutoka kwa Hazina ya Usawazishaji; na
  (b) itakayokuwa kwa muundo, na kwa mujibu wa utaratibu ufaao na kuambatana na
  kanuni zilizoratibiwa na Sheria ya Bunge.
(3) Baraza la Kitaifa litazingatia makadirio yaliyowasilishwa chini ya kifungu cha (1)
pamoja na makadirio yanayowasilishwa na Tume ya Huduma za Bunge na Msajili
Mkuu wa Mahakama chini ya Kifungu cha 127 na 173, mtawalia.
(4) Kabla ya Baraza la Kitaifa kuzingatia makadirio ya mapato na matumizi; kamati
ya Bunge itajadili na kuchunguza makadirio hayo na kutoa mapendekezo yake kwa
Bunge.
(5) Katika kujadili na kuchunguza makadirio hayo, kamati itahusisha umma na
mapendekezo yake yatatiliwa maanani wakati kamati hiyo itakapowasilisha
mapendekezo hayo kwa Baraza la Kitaifa.
(6) Wakati makadirio ya matumizi ya serikali ya kitaifa, makadirio ya matumizi ya
mahakama na Baraza la Kitaifa, yatakuwa yameidhinishwa na Baraza la Kitaifa,
yatajumlishwa katika Mswada wa Matumizi ya Fedha, utakaowasilishwa kwa Baraza
la Kitaifa ili kuidhinisha kutolewa kwa fedha za matumizi kutoka kwa Mfuko wa
Jumla, na matumizi ya fedha hizo kwa madhumuni yaliyotajwa katika mswada.
(7) Mswada wa matumizi ya fedha uliotajwa katika ibara ya (6) hautajumlisha matumizi
yanayodaiwa kutoka kwa Mfuko wa Jumla na Katiba hii au Sheria ya Bunge.
Kwa maneno rahisi
  • Angalau miezi miwili kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha, Katibu wa Baraza la Mawaziri anayeshughulikia fedha huwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa Bunge la Kitaifa.
    Art. 221(1)

    (1) Kwa kipindi kisichopungua miezi miwili kabla ya kukamilika kwa kila mwaka wa kifedha, waziri anayehusika na fedha, atawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka ufuatao wa fedha kwa Baraza la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Kamati ya Bunge hujadili na kupitia makadirio, ikitafuta maoni ya umma.
    Art. 221(5)

    (5) Katika kujadili na kuchunguza makadirio hayo, kamati itahusisha umma na mapendekezo yake yatatiliwa maanani wakati kamati hiyo itakapowasilisha mapendekezo hayo kwa Baraza la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Makadirio yaliyoidhinishwa huwekwa katika Mswada wa Ugavi ili kuidhinisha utoaji kutoka Mfuko wa Pamoja.
    Art. 221(6)

    (6) Wakati makadirio ya matumizi ya serikali ya kitaifa, makadirio ya matumizi ya mahakama na Baraza la Kitaifa, yatakuwa yameidhinishwa na Baraza la Kitaifa, yatajumlishwa katika Mswada wa Matumizi ya Fedha, utakaowasilishwa kwa Baraza la Kitaifa ili kuidhinisha kutolewa kwa fedha za matumizi kutoka kwa Mfuko wa Jumla, na matumizi ya fedha hizo kwa madhumuni yaliyotajwa katika mswada.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kila mwaka, waziri wa fedha huwasilisha bajeti Bungeni, ambalo huipitia na kuidhinisha matumizi.
    Art. 221(1)

    (1) Kwa kipindi kisichopungua miezi miwili kabla ya kukamilika kwa kila mwaka wa kifedha, waziri anayehusika na fedha, atawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka ufuatao wa fedha kwa Baraza la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →