Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12, Sehemu 5 · Art. 223

Matumizi ya Ziada

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kwa kuzingatia ibara ya (2) hadi (4), serikali ya kitaifa inaweza kutumia fedha
ambazo hazijaidhinishwa iwapo –
  (a) Fedha zilizotengwa kwa madhumuni fulani katika sheria ya matumizi
  hazikutosha au kumezuka haja ya matumizi ambayo hayakuwa na mgao katika sheria
  ya matumizi ya fedha; au
  (b) fedha zimechukuliwa kutoka kwenye Hazina ya Ziada ya fedha.
(2) Idhini ya Bunge ya kutumia fedha chini ya kifungu hiki itahitajika kati ya miezi
miwili baada ya fedha kuchukuliwa mara ya kwanza, kulingana na ibara ya (3).
(3) Iwapo Bunge litakuwa limevunjwa wakati wa kipindi kinachotajwa katika ibara ya
(2), au vikao vya bunge vinaendelea na bunge kuvunjwa kabla ya idhini kutolewa,
idhini lazima itolewe kati ya majuma mawili pindi tu vikao vingine vitakapoanza.
(4) Wakati Baraza la Kitaifa litakapokuwa limeidhinisha matumizi chini ya ibara ya (2),
mswada na matumizi ya fedha utawasilishwa kwa mgao wa fedha zilizotumika.
(5) Katika mwaka wowote wa matumizi ya fedha za serikali, serikali ya kitaifa chini ya
kifungu hiki haiwezi kutumia zaidi ya asilimia kumi ya fedha zilizotengewa bunge
kwa mwaka huo, ila katika hali maalum Bunge limeidhisha kiasi cha juu .
Kwa maneno rahisi
  • Serikali ya kitaifa inaweza kutumia fedha zisizoidhinishwa kama kiasi hakitoshi au kuna uhitaji mpya, au fedha zimetolewa kutoka Mfuko wa Dharura.
    Art. 223(1)

    (1) Kwa kuzingatia ibara ya (2) hadi (4), serikali ya kitaifa inaweza kutumia fedha ambazo hazijaidhinishwa iwapo – (a) Fedha zilizotengwa kwa madhumuni fulani katika sheria ya matumizi hazikutosha au kumezuka haja ya matumizi ambayo hayakuwa na mgao katika sheria ya matumizi ya fedha; au (b) fedha zimechukuliwa kutoka kwenye Hazina ya Ziada ya fedha.

    Soma kifungu kamili →
  • Idhini ya Bunge lazima itafutwe ndani ya miezi miwili baada ya utoaji wa kwanza.
    Art. 223(2)

    (2) Idhini ya Bunge ya kutumia fedha chini ya kifungu hiki itahitajika kati ya miezi miwili baada ya fedha kuchukuliwa mara ya kwanza, kulingana na ibara ya (3).

    Soma kifungu kamili →
  • Katika mwaka wa fedha, serikali ya kitaifa haiwezi kutumia zaidi ya asilimia 10 chini ya Kifungu hiki isipokuwa Bunge liidhinishe asilimia kubwa zaidi.
    Art. 223(5)

    (5) Katika mwaka wowote wa matumizi ya fedha za serikali, serikali ya kitaifa chini ya kifungu hiki haiwezi kutumia zaidi ya asilimia kumi ya fedha zilizotengewa bunge kwa mwaka huo, ila katika hali maalum Bunge limeidhisha kiasi cha juu .

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Matumizi ya ziada ya dharura lazima yaidhinishwe na Bunge hivi karibuni.
    Art. 223(2)

    (2) Idhini ya Bunge ya kutumia fedha chini ya kifungu hiki itahitajika kati ya miezi miwili baada ya fedha kuchukuliwa mara ya kwanza, kulingana na ibara ya (3).

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →