Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 12, Sehemu 6 · Art. 227

Ununuzi wa bidhaa na huduma za umma.

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Wakati kitengo cha serikali au shirika lolote la umma linaponunua bidhaa au
huduma, ununizi huo utafanywa kwa njia ya haki, usawa, uwazi, yenye ushindani na
ya kupunguza gharama.
(2) Sheria ya Bunge itatoa mwongozo wa jinsi sera zinazohusishwa na ununuzi na uuzaji
wa mali zitavyotekelezwa na itaamuru kuzingatiwa kwa suala mojawepo au masuala
yote yafuatayo –
  (a) vigezo vya kupewa kipaumbele wakati wa kutoa idhini za ununizi;
  (b) kuwalinda na kuwatetea watu, au makundi ya watu ambao awali walinyanyaswa
  na ushindani usio na haki au uliowatenga;.
  (c) kuweka vikwazo dhidi ya wanakandarasi ambao utendakazi wao hautimizi
  viwango vilivyokubaliwa kitaaluma, kimapatano au kisheria; na
  (d) kuweka vikwazo dhidi ya watu wanaokiuka ulipaji kodi, au ambao wamehusika
  kwenye ufisadi au wenye makosa makubwa ya ukiukaji wa sheria za uajiri kwa haki.
Kwa maneno rahisi
  • Chombo cha umma kinaponunua bidhaa au huduma, lazima kifanye hivyo kwa mfumo wa haki, usawa, uwazi, ushindani na gharama nafuu.
    Art. 227(1)

    (1) Wakati kitengo cha serikali au shirika lolote la umma linaponunua bidhaa au huduma, ununizi huo utafanywa kwa njia ya haki, usawa, uwazi, yenye ushindani na ya kupunguza gharama.

    Soma kifungu kamili →
  • Sheria ya Bunge huweka mfumo wa ununuzi na uuzaji wa mali, ikiwemo upendeleo kwa makundi yaliyotengwa awali.
    Art. 227(2)

    (2) Sheria ya Bunge itatoa mwongozo wa jinsi sera zinazohusishwa na ununuzi na uuzaji wa mali zitavyotekelezwa na itaamuru kuzingatiwa kwa suala mojawepo au masuala yote yafuatayo – (a) vigezo vya kupewa kipaumbele wakati wa kutoa idhini za ununizi; (b) kuwalinda na kuwatetea watu, au makundi ya watu ambao awali walinyanyaswa na ushindani usio na haki au uliowatenga;. (c) kuweka vikwazo dhidi ya wanakandarasi ambao utendakazi wao hautimizi viwango vilivyokubaliwa kitaaluma, kimapatano au kisheria; na (d) kuweka vikwazo dhidi ya watu wanaokiuka ulipaji kodi, au ambao wamehusika kwenye ufisadi au wenye makosa makubwa ya ukiukaji wa sheria za uajiri kwa haki.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Serikali inaponunua vitu, lazima ifanye kwa haki na uwazi.
    Art. 227(1)

    (1) Wakati kitengo cha serikali au shirika lolote la umma linaponunua bidhaa au huduma, ununizi huo utafanywa kwa njia ya haki, usawa, uwazi, yenye ushindani na ya kupunguza gharama.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →