Sura 12, Sehemu 7 · Art. 228
Msimamizi wa Bajeti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kutakuwa na Msimamizi wa Bajeti atakayependekezwa na Rais, kuidhinishwa na Baraza la Kitaifa na kuteuliwa na Rais. (2) Mtu atakayehitimu kuwa Msimamizi, lazima awe na ujuzi mkubwa wa masuala ya fedha za umma au tajriba isiyopungua ya miaka kumi katika ukaguzi na usimamizi wa fedha za umma. (3) Msimamizi wa Bajeti, chini ya Kifungu cha 251, atahudumu kwa kipindi cha miaka nane na hataweza kuteuliwa tena. (4) Msimamizi wa Bajeti atasimamia utekelezaji wa bajeti ya kitaifa na bajeti za serikali za kaunti kwa kuagiza kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma chini ya Kifungu cha 204, 206 na 207. (5) Msimamizi huyu hataidhinisha kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma mpaka aridhike kuwa utowaji huo umekubalika kisheria. (6) Kila baada ya miezi minne, Msimamizi huyu atawasilisha kwa mabaraza yote ya Bunge ripoti ya utekelezaji wa bajeti ya kitaifa na bajeti za serikali za kaunti.
Kwa maneno rahisi
- Kuna Mdhibiti wa Bajeti, anayependekezwa na Rais na kuteuliwa kwa idhini ya Bunge la Kitaifa.
Art. 228(1)
(1) Kutakuwa na Msimamizi wa Bajeti atakayependekezwa na Rais, kuidhinishwa na Baraza la Kitaifa na kuteuliwa na Rais.
Soma kifungu kamili → - Mdhibiti husimamia utekelezaji wa bajeti kwa kuidhinisha utoaji wa fedha za umma.
Art. 228(4)
(4) Msimamizi wa Bajeti atasimamia utekelezaji wa bajeti ya kitaifa na bajeti za serikali za kaunti kwa kuagiza kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma chini ya Kifungu cha 204, 206 na 207.
Soma kifungu kamili → - Mdhibiti hawezi kuidhinisha utoaji isipokuwa aridhike kwamba umeruhusiwa na sheria.
Art. 228(5)
(5) Msimamizi huyu hataidhinisha kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma mpaka aridhike kuwa utowaji huo umekubalika kisheria.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Afisa huhakikisha fedha za umma zinatolewa tu pale sheria inaruhusu.
Art. 228(4)
(4) Msimamizi wa Bajeti atasimamia utekelezaji wa bajeti ya kitaifa na bajeti za serikali za kaunti kwa kuagiza kutolewa kwa fedha kutoka kwa hazina za umma chini ya Kifungu cha 204, 206 na 207.
Soma kifungu kamili →