Sura 12, Sehemu 7 · Art. 231
Benki Kuu ya Kenya
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Benki Kuu ya Kenya imeundwa. (2) Benki Kuu ya Kenya inawajibikia kuelekeza sera za kifedha, kudumisha udhabiti wa bei, kutoa sarafu na kutekeleza majukumu mengine kama yalivyotolewa na sheria ya Bunge. (3) Benki Kuu ya Kenya haitakuwa chini ya mamlaka au kuelekezwa na mtu au shirika lolote inapokuwa inatumia mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake. (4) Noti na sarafu zinazotolewa na Benki Kuu ya Kenya zinaweza kuwa na picha zinazoashiria Kenya au kifungu cha Kenya lakini zisiwe na picha ya mtu yeyote. (5) Sheria ya Bunge itatoa mwongozo, wahusika, mamlaka, majukumu na utendakazi wa Benki Kuu ya Kenya.
Kwa maneno rahisi
- Kuna Benki Kuu ya Kenya.
Art. 231(1)
(1) Benki Kuu ya Kenya imeundwa.
Soma kifungu kamili → - Hutunga sera ya fedha, hukuza uthabiti wa bei na kutoa sarafu.
Art. 231(2)
(2) Benki Kuu ya Kenya inawajibikia kuelekeza sera za kifedha, kudumisha udhabiti wa bei, kutoa sarafu na kutekeleza majukumu mengine kama yalivyotolewa na sheria ya Bunge.
Soma kifungu kamili → - Haiko chini ya maelekezo au udhibiti wa mtu yeyote au mamlaka yoyote.
Art. 231(3)
(3) Benki Kuu ya Kenya haitakuwa chini ya mamlaka au kuelekezwa na mtu au shirika lolote inapokuwa inatumia mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Benki Kuu hutunza fedha za Kenya na kudumisha uthabiti wa bei.
Art. 231(2)
(2) Benki Kuu ya Kenya inawajibikia kuelekeza sera za kifedha, kudumisha udhabiti wa bei, kutoa sarafu na kutekeleza majukumu mengine kama yalivyotolewa na sheria ya Bunge.
Soma kifungu kamili →