Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 13, Sehemu 2 · Art. 233

Tume ya Huduma za Umma

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Tume imeundwa ya Huduma za Umma.
(2) Tume ya Huduma za Umma inahusisha mwenyekiti, naibu wa mwenyekiti na
wanachama wengine saba walioteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Baraza Kuu la
Kitaifa.
(3) Kwa mujibu wa ibara ya (4), mtu hastahili kuteuliwa kama mwanachama wa Tume
hii iwapo mtu huyo-
  (a) kwa kipindi cha miaka mitano iliyotangulia alikuwa na afisi au amewania kiti
  katika uchaguzi kama-
  (i) mwanachama wa bunge au wa baraza la kaunti; au
  (ii) mwanachama katika bodi ya uongozi ya chama cha kisiasa;
  au
  (b) ana wadhifa katika afisi yoyote ya serikali;
  (c) anagombea kiti, au kwa wakati wowote amewahi kugombea kiti cha ubunge au
  katika baraza la kaunti; au
  (d) anashikilia, au kwa wakati wowote ule, amewahi kushikilia kiti cha afisi ya
  shirika la kisiasa linalofadhili au kuunga mkono mgombeaji wa ubunge au wa baraza
  la kaunti.
(4) ibara ya (3) (c) na (d) hazitatumika iwapo uchaguzi mkuu umefanywa mara mbili
tangu mtu huyo alipogombea kiti au alipokuwa afisini.
(5) Kutakuwa na katibu wa Tume.
(6) Katibu wa Tume-
  (i) ndiye afisa mkuu wa Tume; na
  (ii) atateuliwa na Tume kwa kipindi cha miaka mitano na anaweza kuteuliwa
  upya mara moja tu.
Kwa maneno rahisi
  • Kuna Tume ya Huduma za Umma, inayoundwa na mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wengine saba walioteuliwa na Rais kwa idhini ya Bunge la Kitaifa.
    Art. 233(2)

    (2) Tume ya Huduma za Umma inahusisha mwenyekiti, naibu wa mwenyekiti na wanachama wengine saba walioteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Baraza Kuu la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Mjumbe hapaswi kuwa ameshikilia ofisi ya kisiasa au kiti cha ubunge katika miaka mitano iliyopita.
    Art. 233(3)

    (3) Kwa mujibu wa ibara ya (4), mtu hastahili kuteuliwa kama mwanachama wa Tume hii iwapo mtu huyo- (a) kwa kipindi cha miaka mitano iliyotangulia alikuwa na afisi au amewania kiti katika uchaguzi kama- (i) mwanachama wa bunge au wa baraza la kaunti; au (ii) mwanachama katika bodi ya uongozi ya chama cha kisiasa; au (b) ana wadhifa katika afisi yoyote ya serikali; (c) anagombea kiti, au kwa wakati wowote amewahi kugombea kiti cha ubunge au katika baraza la kaunti; au (d) anashikilia, au kwa wakati wowote ule, amewahi kushikilia kiti cha afisi ya shirika la kisiasa linalofadhili au kuunga mkono mgombeaji wa ubunge au wa baraza la kaunti.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Tume husimamia uteuzi katika huduma za umma.
    Art. 233(1)

    (1) Tume imeundwa ya Huduma za Umma.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →