Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 13, Sehemu 2 · Art. 234

Majukumu na Mamlaka ya Tume ya Huduma za Umma

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Majukumu na mamlaka ya Tume ni kama yalivyofafanuliwa katika kifungu hiki .
(2) Tume-
  (a) kwa mujibu wa Katiba hii na sheria-
  (i) itaunda na kuvunja afisi katika huduma za umma;
  (ii) itateua watu kuhudumu au kushikilia afisi pamoja na kuthibitisha uteuzi huo.
  (b) itadumisha nidhamu na kuwaondoa kazini maafisa walio katika afisi hizo au
  wanaozishikilia kwa muda;
  (c) itakuza maadili na kanuni zilizotajwa katika Vifungu vya 10 na 232 kote katika
  utoaji wa huduma za umma;
  (d) itachunguza, kufuatilia, na kutathmini usimamizi na mienendo ya wafanyakazi
  katika utoaji wa huduma za umma;
  (e) itahakikisha utendakazi bora katika huduma za umma;
  (f) itakuza uajiri katika huduma za umma;
  (g) itachunguza na kutoa mapendekezo kwa serikali ya kitaifa kuhusu hali za
  utendakazi, kanuni za utendakazi, na ustahili wa maafisa wanaotoa huduma za
  umma;
  (h) itatathmini na kuripoti kwa Rais na Bunge kuhusu kiwango ambacho maadili na
  kanuni zilizotajwa katika Vifungu vya 10 na 232 zinazingatiwa katika huduma za
  umma;
  (i) itasikiza na kuamua rufani kuhusu masuala yanayohusiana na huduma za umma
  katika serikali za kaunti;
  (j) itatekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote kama ilivyopewa na sheria ya nchi.
(3) ibara ya (1) na (2) hazitatekelezwa katika afisi zozote zifuatazo za huduma za
umma-
  (a) afisi za Serikali;
  (b) afisi ya Balozi wa nchi za Jumuia ya madola, balozi au mwakilishi yeyote katika
  afisi za kibalozi za Jamhuri;
  (c) afisi au wadhifa kwa mujibu wa-
  (i) Tume ya Huduma za Bunge;
  (ii) Tume ya Huduma za Mahakama;
  (iii) Tume ya kuwaajiri walimu; au
  (iv) Tume ya Huduma za Polisi ya Kitaifa; au
  (d) afisi inayohudumia serikali ya kaunti, isipokuwa ilivyofafanuliwa katika ibara ya
(2) (i).
(4) Chini ya ibara ya (2), Tume haitamteua mtu kuchukua wadhifa au kushikilia afisi
kama mfanyikazi katika afisi ya Rais au ya Rais mstaafu mpaka pawe na kibali
kutoka kwa Rais au Rais mstaafu.
(5) Kupitia kwa maandishi, Tume inaweza, kwa masharti au bila ya masharti, kukabidhi
majukumu na mamlaka yake yoyote chini ya Kifungu hiki kwa yeyote kati ya
wanachama wake, au kwa afisa yeyote, bodi au idara katika huduma za umma.
Kwa maneno rahisi
  • Tume ya Huduma za Umma huanzisha ofisi katika huduma za umma na huteua watu kushikilia ofisi hizo.
    Art. 234(2)(a)

    (a) kwa mujibu wa Katiba hii na sheria-

    Soma kifungu kamili →
  • Hutumia udhibiti wa kinidhamu na inaweza kuwaondoa watu wanaoshikilia ofisi hizo.
    Art. 234(2)(b)

    (b) itadumisha nidhamu na kuwaondoa kazini maafisa walio katika afisi hizo au wanaozishikilia kwa muda;

    Soma kifungu kamili →
  • Hukuza maadili na kanuni zilizo katika Vifungu vya 10 na 232 katika huduma za umma.
    Art. 234(2)(c)

    (c) itakuza maadili na kanuni zilizotajwa katika Vifungu vya 10 na 232 kote katika utoaji wa huduma za umma;

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Tume huajiri, hupandisha vyeo na kuadhibu watendaji wa umma.
    Art. 234(2)

    (2) Tume- (a) kwa mujibu wa Katiba hii na sheria- (i) itaunda na kuvunja afisi katika huduma za umma; (ii) itateua watu kuhudumu au kushikilia afisi pamoja na kuthibitisha uteuzi huo. (b) itadumisha nidhamu na kuwaondoa kazini maafisa walio katika afisi hizo au wanaozishikilia kwa muda; (c) itakuza maadili na kanuni zilizotajwa katika Vifungu vya 10 na 232 kote katika utoaji wa huduma za umma; (d) itachunguza, kufuatilia, na kutathmini usimamizi na mienendo ya wafanyakazi katika utoaji wa huduma za umma; (e) itahakikisha utendakazi bora katika huduma za umma; (f) itakuza uajiri katika huduma za umma; (g) itachunguza na kutoa mapendekezo kwa serikali ya kitaifa kuhusu hali za utendakazi, kanuni za utendakazi, na ustahili wa maafisa wanaotoa huduma za umma; (h) itatathmini na kuripoti kwa Rais na Bunge kuhusu kiwango ambacho maadili na kanuni zilizotajwa katika Vifungu vya 10 na 232 zinazingatiwa katika huduma za umma; (i) itasikiza na kuamua rufani kuhusu masuala yanayohusiana na huduma za umma katika serikali za kaunti; (j) itatekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote kama ilivyopewa na sheria ya nchi.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →