Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 14, Sehemu 1 · Art. 239

Idara za usalama wa kitaifa

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Idara za usalama wa kitaifa ni -
  (a) Vikosi vya Ulinzi wa Kenya;
  (b) Huduma za Upelelezi za kitaifa; na
  (c) Huduma za Polisi za kitaifa.
(2) Lengo la kimsingi la idara za usalama wa kitaifa na utaratibu wa usalama ni
kuendeleza na kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa kitaifa kwa mujibu wa kanuni
zilizotajwa katika Kifungu cha 238(2).
(3) Katika kutekeleza majukumu na mamlaka yao, idara za usalama wa kitaifa na kila
mwanachama wa idara hizo hataruhusiwa -
  (a) kuwa na upendeleo kwa njia yoyote,
  (b) kuendeleza maslahi ya chama chochote cha kisiasa wala sera zake; au
  (c) kuhujumu maslahi ya kisiasa au sera zake za kisiasa ambazo ni halali chini ya
  Katiba hii.
(4) Mtu hataruhusiwa kubuni kikosi cha kijeshi au kikosi chenye hadhi ya kijeshi
au shirika linalodai kuendeleza na kuhakikisha usalama wa kitaifa isipokuwa
inavyoruhusiwa na Katiba hii au Sheria ya Bunge.
(5) Idara za uslama wa kitaifa zitakuwa chini ya mamlaka ya raia.
(6) Bunge litatunga sheria kushughulikia majukumu, utaratibu na usimamizi wa idara za
usalama wa kitaifa.
Kwa maneno rahisi
  • Vyombo vya usalama vya kitaifa ni Jeshi la Ulinzi la Kenya, Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi na Huduma ya Polisi ya Kitaifa.
    Art. 239(1)

    (1) Idara za usalama wa kitaifa ni - (a) Vikosi vya Ulinzi wa Kenya; (b) Huduma za Upelelezi za kitaifa; na (c) Huduma za Polisi za kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Lengo lao kuu ni kukuza na kuhakikisha usalama wa kitaifa kwa kufuata kanuni za Kifungu cha 238(2).
    Art. 239(2)

    (2) Lengo la kimsingi la idara za usalama wa kitaifa na utaratibu wa usalama ni kuendeleza na kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa kitaifa kwa mujibu wa kanuni zilizotajwa katika Kifungu cha 238(2).

    Soma kifungu kamili →
  • Hawapaswi kutenda kwa upendeleo wa kisiasa au kuendeleza maslahi ya chama cha siasa.
    Art. 239(3)

    (3) Katika kutekeleza majukumu na mamlaka yao, idara za usalama wa kitaifa na kila mwanachama wa idara hizo hataruhusiwa - (a) kuwa na upendeleo kwa njia yoyote, (b) kuendeleza maslahi ya chama chochote cha kisiasa wala sera zake; au (c) kuhujumu maslahi ya kisiasa au sera zake za kisiasa ambazo ni halali chini ya Katiba hii.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Vyombo vya usalama vya Kenya ni jeshi, idara ya ujasusi na polisi.
    Art. 239(1)

    (1) Idara za usalama wa kitaifa ni - (a) Vikosi vya Ulinzi wa Kenya; (b) Huduma za Upelelezi za kitaifa; na (c) Huduma za Polisi za kitaifa.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →