Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 14, Sehemu 4 · Art. 246

Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa imeundwa.
(2) Tume inahusisha–
  (a) watu wafuatao, kila mmoja wao akiwa ameteuliwa na Rais-
  (i) mtu anayestahili kuteuliwa kama Jaji wa Mahakama ya Juu;
  (ii) maafisa wawili wa polisi wa ngazi za juu waliostaafu; na
  (iii) watu watatu wenye maadili mema ambao wamewahi kuhudumu serikalini
  kwa umahiri mkubwa.
  (b) Inspekta-Mkuu wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
  (c) Manaibu wote wawili wa Inspekta-Mkuu wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
(3) Tume -
  (a) itaajiri na kuteua watu kuhudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma
  hiyo, kuidhinisha uteuzi na kuamua watakaopandishwa vyeo na kuhamishwa katika
  huduma za polisi za kitaifa.
  (b) itazingatia utaratibu wa sheria, kutekeleza majukumu ya kinidhamu na
  kuwaondoa watu wanaohudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hii; na
  (c) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa sheria ya nchi..
(4) Uajiri katika Huduma za Polisi za Kitaifa utabainisha tofauti za kimaeneo na za
jamii mbalimbali za watu wa Kenya.
Kwa maneno rahisi
  • Kuna Tume ya Huduma ya Polisi ya Kitaifa.
    Art. 246(1)

    (1) Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa imeundwa.

    Soma kifungu kamili →
  • Huaajiri na huteua watu kushikilia ofisi katika huduma, huamua upandishaji na uhamishaji, na hutumia udhibiti wa kinidhamu.
    Art. 246(3)

    (3) Tume - (a) itaajiri na kuteua watu kuhudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hiyo, kuidhinisha uteuzi na kuamua watakaopandishwa vyeo na kuhamishwa katika huduma za polisi za kitaifa. (b) itazingatia utaratibu wa sheria, kutekeleza majukumu ya kinidhamu na kuwaondoa watu wanaohudumu au kushikilia kwa muda afisi za huduma hii; na (c) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa sheria ya nchi..

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Tume husimamia uajiri, upandishaji na nidhamu ya polisi.
    Art. 246(1)

    (1) Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa imeundwa.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →