Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 15 · Art. 251

Kuondolewa afisini

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mwanachama wa Tume (isipokuwa aliye mwanachama kutokana na wadhifa wake) ,
au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru, anaweza kuondolewa afisini kwa sababu ya-
  (a) ukiukaji uliokithiri wa Katiba hii au sheria yoyote ikiwa ni pamoja na kuvunja
  sheria katika sura ya sita;
  (b) utovu wa nidhamu ama ni katika utendakazi wa mwanachama au yule
  anayeshikilia wadhifa wa afisi huru;
  (c) kutokuwa na uwezo wa kimwili au kiakili katika kutekeleza majukumu ya kiafisi;
  (d) kushindwa kufanya kazi; au
  (e) kufilisika.
(2) Mtu anayeazimia kuondolewa kwa mwanachama wa tume au anayeshikilia wadhifa
wa afisi huru kwa misingi yoyote iliyotajwa katika ibara ya (1) anaweza kuwasilisha
malalamiko kwa Baraza la Bunge huku akifafanua yale yote yanayothibitisha azma hiyo.
(3) Baraza la Bunge litachunguza malalamiko hayo na , iwapo litaridhika kwamba
yana mashiko chini ya ibara ya (1), litatuma malalamiko hayo kwa Rais.
(4) Pindi tu baada ya kupokea malalamiko hayo chini ya ibara ya (3),Rais –
  (a) anaweza kumsimamisha kazi mwanachama wa tume au anayeshikiia wadhifa wa
  afisi huru huku akisubiri matokeo ya uchunguzi wa malalamiko hayo; na
  (b) atateua mahakama maalum kulingana na ibara ya (5).
(5) Mahakama hii maalum itahusisha –
  (a) mtu ambaye anahudumu, au amewahi kuhudumu kama jaji wa mahakama yenye
  mamlaka makuu, ambaye pia atakuwa mwenyekiti;
  (b) angalau watu wawili ambao wanastahili kuteuliwa kama majaji wa Mahakama
  ya Juu; na
  (c) mwanachama mwingine mmoja ambaye ana uwezo wa kuchunguza ushahidi
  kuhusiana na msingi mahususi wa kumtaka afisa huyo aondolewe.
(6) Mahakama maluum itachunguza suala hilo kwa haraka, na kutoa ripoti ya matokeo
na mapendekezo yenye mashiko kwa Rais, ambaye atachukua hatua kulingana na
mapendekezo hayo katika kipindi cha siku thelathini.
(7) Mtu atakayesimamishwa kazi chini ya Kifungu hiki ana haki ya kuendelea kupokea
nusu ya zawadi na faida ya afisi akiwa amesimamishwa kazi.
Kwa maneno rahisi
  • Mjumbe wa tume au mshikiliaji wa ofisi huru anaweza kuondolewa tu kwa ukiukaji mkubwa wa Katiba au sheria, maovu makubwa, kutokuwa na uwezo, kukosa umahiri, au kufilisika.
    Art. 251(1)

    (1) Mwanachama wa Tume (isipokuwa aliye mwanachama kutokana na wadhifa wake) , au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru, anaweza kuondolewa afisini kwa sababu ya- (a) ukiukaji uliokithiri wa Katiba hii au sheria yoyote ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria katika sura ya sita; (b) utovu wa nidhamu ama ni katika utendakazi wa mwanachama au yule anayeshikilia wadhifa wa afisi huru; (c) kutokuwa na uwezo wa kimwili au kiakili katika kutekeleza majukumu ya kiafisi; (d) kushindwa kufanya kazi; au (e) kufilisika.

    Soma kifungu kamili →
  • Mtu anaweza kuwasilisha ombi kwa Bunge la Kitaifa, ambalo linaweza kulipeleka kwa Rais, ambaye huteua kamati kuchunguza.
    Art. 251(2)

    (2) Mtu anayeazimia kuondolewa kwa mwanachama wa tume au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru kwa misingi yoyote iliyotajwa katika ibara ya (1) anaweza kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la Bunge huku akifafanua yale yote yanayothibitisha azma hiyo.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kamishna anaweza kuondolewa kwa sababu kubwa tu, baada ya uchunguzi.
    Art. 251(1)

    (1) Mwanachama wa Tume (isipokuwa aliye mwanachama kutokana na wadhifa wake) , au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru, anaweza kuondolewa afisini kwa sababu ya- (a) ukiukaji uliokithiri wa Katiba hii au sheria yoyote ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria katika sura ya sita; (b) utovu wa nidhamu ama ni katika utendakazi wa mwanachama au yule anayeshikilia wadhifa wa afisi huru; (c) kutokuwa na uwezo wa kimwili au kiakili katika kutekeleza majukumu ya kiafisi; (d) kushindwa kufanya kazi; au (e) kufilisika.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →