Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 15 · Art. 252

Majukumu na Mamlaka ya jumla

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kila tume, na anayeshikilia wadhifa wa afisi huru –
  (a) anaweza kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi au kufuatia malalamiko
  yaliyotolewa na mwananchi;
  (b) ana mamlaka muhimu ya kupatanisha , kusuluhisha na kujadiliana ili kupata
  maafikiano;
  (c) itaajiri wafanyakazi wake; na
  (d) inaweza kutekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote iliyopewa na sheria,
  mbali na majukumu na mamlaka iliyopewa na Katiba hii.
(2) Malalamiko kwa Tume au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru yanaweza
kuwasilishwa na mtu yeyote mwenye kibali cha kuendeleza mashtaka chini ya
kifungu cha 22 (1) na (2) .
(3) Tume na afisi huru zifuatazo zina mamlaka ya kumwita shahidi kutoa usaidizi kwa
madhumuni ya kufanya uchunguzi wao-
  (a) Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa ya Kenya;
  (b) Tume ya Huduma za Mahakama;
  (c) Tume ya Kitaifa ya Ardhi;
  (d) Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.
Kwa maneno rahisi
  • Kila tume inaweza kufanya uchunguzi kwa hiari yake au kwa malalamiko ya mwananchi.
    Art. 252(1)(a)

    (a) anaweza kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi au kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mwananchi;

    Soma kifungu kamili →
  • Ina mamlaka ya upatanishi, usuluhishi na mazungumzo, na huajiri wafanyakazi wake.
    Art. 252(1)(b)

    (b) ana mamlaka muhimu ya kupatanisha , kusuluhisha na kujadiliana ili kupata maafikiano;

    Soma kifungu kamili →
  • Tume zingine, ikiwemo Tume ya Haki za Binadamu na Usawa na Tume ya Kitaifa ya Ardhi, na Mkaguzi Mkuu, zinaweza kutoa wito kwa mashahidi.
    Art. 252(3)

    (3) Tume na afisi huru zifuatazo zina mamlaka ya kumwita shahidi kutoa usaidizi kwa madhumuni ya kufanya uchunguzi wao- (a) Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa ya Kenya; (b) Tume ya Huduma za Mahakama; (c) Tume ya Kitaifa ya Ardhi; (d) Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Tume zinaweza kuchunguza malalamiko na kusaidia kutatua migogoro.
    Art. 252(1)

    (1) Kila tume, na anayeshikilia wadhifa wa afisi huru – (a) anaweza kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi au kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mwananchi; (b) ana mamlaka muhimu ya kupatanisha , kusuluhisha na kujadiliana ili kupata maafikiano; (c) itaajiri wafanyakazi wake; na (d) inaweza kutekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote iliyopewa na sheria, mbali na majukumu na mamlaka iliyopewa na Katiba hii.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →