Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 16 · Art. 257

Marekebisho yanayotokana na juhudi za wengi

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Marekebisho ya Katiba hii yanaweza kupendekezwa kutokana na juhudi za wengi
ikiwa angalau watu milioni moja waliojiandikisha kupiga kura wametia sahihi.
(2) Juhudi za wengi za marekebisho ya Katiba hii zinaweza kuchukua muundo wa
pendekezo la jumla au kupitia kwa rasimu ya Mswada iliyotayarishwa.
(3) Iwapo juhudi za wengi zitahusisha kupitia kwa njia ya pendekezo la jumla,
wanaoendeleza pendekezo hili watalitayarisha liwe kama rasimu ya Mswada kupitia
kwa wadhamini wao.
(4) Wadhamini wanaoendeleza juhudi za wengi watawasilisha rasimu ya Mswada
pamoja na sahihi walizokusanya kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ambayo
itathibitisha kwamba pendekezo hilo linaungwa mkono na angalau na wapiga kura
milioni moja waliosajiliwa.
(5) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itakaporidhika kwamba pendekezo hilo
limetimiza masharti ya Kifungu hiki, Tume hii itawasilisha pendekezo hilo kwa
kila baraza la kaunti ili kujadiliwa katika muda wa miezi mitatu baada ya tarehe ya
kuwasilishwa na Tume hiyo.
(6) Iwapo baraza la kaunti litaidhinisha rasimu ya Mswada katika kipindi cha miezi
mitatu tangu tarehe ilipowasilishwa na Tume, Spika wa baraza la kaunti atawasilisha
nakala ya rasimu ya Mswada kwa Maspika wawili wa viwango vyote viwili vya
Bunge, pamoja na cheti kwamba baraza la kaunti limeidhinisha.
(7) Iwapo rasimu ya Mswada imeidhinishwa na mabaraza mengi ya kaunti, rasimu hiyo
itawasilishwa Bungeni bila kuchelewa.
(8) Chini ya kifungu hiki, Mswada utaidhinishwa na Bunge iwapo utaungwa mkono na
wabunge wengi katika kila kiwango cha Bunge.
(9) Iwapo Bunge litaupitisha Mswada huo, utapelekewa Rais kutiwa sahihi kulingana na
Kifungu cha 256 (4) na (5).
(10) Iwapo kila ngazi ya Bunge haitapitisha Mswada, au Mswada huo unahusu suala
lililotajwa katika kifungu cha 255 (1), Mswada huo uliopendekezwa utapalekwa
kwa watu kwa kura ya maamuzi
(11) Kifungu cha 255 (2) kitatumika, kukiwemo na marekebisho muhimu yoyote, katika
kura ya maamuzi chini ya ibara ya (10).
Kwa maneno rahisi
  • Marekebisho yanaweza kupendekezwa kwa mwito wa wananchi uliotiwa sahihi na angalau wapiga kura milioni moja waliojiandikisha.
    Art. 257(1)

    (1) Marekebisho ya Katiba hii yanaweza kupendekezwa kutokana na juhudi za wengi ikiwa angalau watu milioni moja waliojiandikisha kupiga kura wametia sahihi.

    Soma kifungu kamili →
  • Sahihi huhakikiwa na IEBC, na rasimu ya Mswada huwasilishwa kwa mabunge ya kaunti kwa kuzingatia.
    Art. 257(4)

    (4) Wadhamini wanaoendeleza juhudi za wengi watawasilisha rasimu ya Mswada pamoja na sahihi walizokusanya kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ambayo itathibitisha kwamba pendekezo hilo linaungwa mkono na angalau na wapiga kura milioni moja waliosajiliwa.

    Soma kifungu kamili →
  • Kama wingi wa mabunge ya kaunti wakiidhinisha, Mswada huwasilishwa Bungeni.
    Art. 257(7)

    (7) Iwapo rasimu ya Mswada imeidhinishwa na mabaraza mengi ya kaunti, rasimu hiyo itawasilishwa Bungeni bila kuchelewa.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Watu wanaweza kupendekeza mabadiliko ya Katiba kama wapiga kura milioni moja wamesaini.
    Art. 257(1)

    (1) Marekebisho ya Katiba hii yanaweza kupendekezwa kutokana na juhudi za wengi ikiwa angalau watu milioni moja waliojiandikisha kupiga kura wametia sahihi.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →