Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 17 · Art. 258

Utekelezaji wa Katiba hii

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa Katiba hii
imekiukwa , au inatishiwa na kukiukwa.
(2) Pamoja na mtu anayefanya hivyo kwa maslahi yake mwenyewe kesi inaweza
kuwasilishwa mahakamani na- kulingana na ibara ya (1)-
  (a) mtu anayewasilisha kwa niaba ya mwingine ambaye hawezi kufanya hivyo yeye
  binafsi;
  (b ) mtu anayewasilisha kama mwanachama wa, au kwa maslahi ya, kundi au
  makundi ya watu;
  (c) mtu anayewasilisha kwa niaba ya maslahi ya umma; au
  (d) chama kinachowasilisha kwa maslahi ya mmoja au zaidi ya wanachama wake.
Kwa maneno rahisi
  • Kila mtu ana haki ya kuanzisha kesi mahakamani akidai kwamba Katiba imekiukwa au inatishiwa kukiukwa.
    Art. 258(1)

    (1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa Katiba hii imekiukwa , au inatishiwa na kukiukwa.

    Soma kifungu kamili →
  • Kesi zinaweza pia kuanzishwa kwa niaba ya mwingine, kikundi, maslahi ya umma, au chama.
    Art. 258(2)

    (2) Pamoja na mtu anayefanya hivyo kwa maslahi yake mwenyewe kesi inaweza kuwasilishwa mahakamani na- kulingana na ibara ya (1)- (a) mtu anayewasilisha kwa niaba ya mwingine ambaye hawezi kufanya hivyo yeye binafsi; (b ) mtu anayewasilisha kama mwanachama wa, au kwa maslahi ya, kundi au makundi ya watu; (c) mtu anayewasilisha kwa niaba ya maslahi ya umma; au (d) chama kinachowasilisha kwa maslahi ya mmoja au zaidi ya wanachama wake.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mtu yeyote anaweza kwenda mahakamani kama Katiba inavunjwa au inakaribia kuvunjwa.
    Art. 258(1)

    (1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa Katiba hii imekiukwa , au inatishiwa na kukiukwa.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →