Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 17 · Art. 259

Kufasiri Katiba hii

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Katiba hii itafasiriwa kwa namna ambayo –
  (a) inakuza malengo, maadili na kanuni zake;
  (b) inaendeleza utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi ulioko
  katika Sheria ya Haki;
  (c) inaruhusu maendeleo ya sheria; na
  (d) inachangia utawala bora.
(2) Iwapo kuna mkinzano kati ya matoleo ya lugha tofauti ya Katiba hii, toleo la lugha
ya Kiingereza ndilo litakalotawala.
(3) kila sharti la Katiba hii litafasiriwa kulingana na kanuni za ufasiri kwamba sheria
kila mara inazungumza, na hivyo basi, miongoni mwa vitu vingine –
  (a) jukumu la mamlaka lililotolewa na Katiba hii kwa afisi linaweza kufanywa au
  kutekelezwa na mtu anayeshikilia wadhifa katika afisi hiyo kama inavyohitajika;
  (b) rejeleo lolote katika Katiba hii kwa serikali au kwa afisi nyingine ya umma au
  afisa, au mtu anayeshilikia afisi hiyo ni rejeleo kwa mtu anayeshikilia afisi hiyo kwa
  muda au anayetekeleza majukumu ya afisi hiyo wakati wowote ule;
  (c) rejeleo katika Katiba hii kwa afisi, idara ya serikali au mahali palipotajwa
  kwenye Katiba hii litasomwa pamoja na badiliko lolote rasmi linalohitajika ili
  likubalike katika mazingira hayo; na
  (d) rejeleo katika Katiba hii kwa afisi, kundi au shirika, ikiwa ni afisi, na iwapo kundi
  au shirika halipo tena, basi yule aliyerithi ndiye atakayerejelewa au yeyote husika
  katika afisi, kundi au shirika.
(4) Katika Katiba hii, isipokuwa pale ambapo muktadha unahitaji vinginevyo-
  (a) iwapo neno au maelezo yamefafanuliwa katika Katiba hii, tofauti zozote za
  kisarufi au matumizi ya neno linalohusiana na jingine, soma ukizingatia mabadiliko
  yanayotokana na muktadha; na
  (b) neno “-kiwemo” linamaanisha “ikiwemo, lakini bila mpaka”;
(5) Katika kuhesabu wakati baina ya matukio mawili kwa shughuli yoyote katika Katiba
hii, kama wakati umeelezwa-
  (a) kama siku, basi siku ambayo tukio la kwanza linatokea haitazingatiwa, na siku
  ambayo tukio la mwisho linaweza kutokea itahusishwa;
  (b) kama miezi, kipindi cha muda uliowekwa huisha mwanzoni mwa siku katika
  mwezi husika-
  (i) ambao una nambari sawa kama tarehe ambapo kipindi hicho kilianza, iwapo
  mwezi huo una tarehe inayolingana; au
  (ii) hiyo ndiyo siku ya mwisho ya mwezi huo; au
  (c) kama miaka, kipindi cha muda huo kinamalizika mwanzoni mwa tarehe ya
  mwaka husika inayolingana na tarehe ambayo kipindi hicho kilianza.
(6) Iwapo muda uliotengwa katika Katiba hii kwa lengo lolote ni siku sita au chini yake,
Jumapili na siku za mapumziko hazitahesabiwa wakati wa kuhesabu muda.
(7) Iwapo, katika hali yoyote maalumu, kipindi cha muda kilichoelezwa na Katiba hii
kinakamilika Jumapili au siku ya mapumziko, muda huo unaongezwa hadi siku
inayofuata ambayo siyo Jumapili au siku ya mapumziko.
(8) Iwapo muda fulani haukuelezwa na Katiba hii ili kuekeleza kitendo fulani, kitendo
hicho kitafanywa bila kuchelewa na kulingana na wakati wowote shughuli hiyo
inapohitajika.
(9) Iwapo mtu yeyote au idara ya Serikali ina mamlaka chini ya Katiba hii kuongeza
kipindi cha muda unaoruhusiwa katika Katiba hii, mamlaka hayo yanaweza
kutekelezwa kabla au baada ya mwisho wa kipindi hicho isipokuwa pale ambapo nia
tofauti imeelezwa wazi katika sharti linalotoa mamlaka hayo.
(10) Isipokuwa pale ambapo Katiba hii inaeleza tofauti, ikiwa mtu ameondoka katika
afisi iliyoundwa na Katiba hii, iwapo mtu huyo anastahili kutokana na umahiri wake
kazini, anaweza kuteuliwa tena, kuchaguliwa kwa kupigiwa kura au vinginevyo
kuchaguliwa tu kuchukua afisi hiyo kulingana na Katiba hii.
(11) Ikiwa jukumu au mamlaka yaliyopewa mtu chini ya Katiba hii hutekelezwa na mtu
huyo tu kupitia kwa ushauri au pendekezo, kupitia kwa kuidhinisha au kukubali kwa,
au kupitia kwa mashauriano na mtu mwingine, jukumu linaweza kufanywa ama
mamlaka kutekelezwa kupitia tu kwa ushauri huo, pendekezo, kwa kuidhinisha au
kukubali huko, au baada ya mashauriano hayo, isipokuwa pale ambapo Katiba hii
inaeleza vinginevyo.
Kwa maneno rahisi
  • Katiba lazima ifasiriwe kwa namna inayokuza malengo, maadili na kanuni zake, kukuza utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi, kuruhusu maendeleo ya sheria, na kuchangia utawala bora.
    Art. 259(1)

    (1) Katiba hii itafasiriwa kwa namna ambayo – (a) inakuza malengo, maadili na kanuni zake; (b) inaendeleza utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki; (c) inaruhusu maendeleo ya sheria; na (d) inachangia utawala bora.

    Soma kifungu kamili →
  • Kama kuna mgongano kati ya matoleo ya lugha, toleo la Kiingereza linatawala.
    Art. 259(2)

    (2) Iwapo kuna mkinzano kati ya matoleo ya lugha tofauti ya Katiba hii, toleo la lugha ya Kiingereza ndilo litakalotawala.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Katiba isomwe kwa namna inayosaidia zaidi haki za watu na utawala bora.
    Art. 259(1)

    (1) Katiba hii itafasiriwa kwa namna ambayo – (a) inakuza malengo, maadili na kanuni zake; (b) inaendeleza utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki; (c) inaruhusu maendeleo ya sheria; na (d) inachangia utawala bora.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →