Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 5, Sehemu 2 · Art. 70

Utekelezwaji wa haki za mazingira

  • Kama haki ya mazingira safi na yenye afya inakataliwa au kutishiwa, mtu anaweza kuomba mahakama ufumbuzi.
    Art. 70(1)

    (1) Iwapo mtu anadai kuwa haki ya kupata mazingira safi na yenye afya inayotambuliwa na kulindwa chini ya Kifungu cha 42 imekiukwa, inakiukwa au inaelekea kukiukwa, kunyimwa, kuvunjwa au kutishiwa, mtu huyo anaweza kuwasilisha kesi mahakamani ili asikilizwe mbali na hatua nyingine za kisheria zitakazoshughulikia suala hilo.

    Soma kifungu kamili →
  • Mahakama inaweza kuamuru vitendo vyenye madhara visimamishwe, au kutoa fidia.
    Art. 70(2)

    (2) Kutokana na ombi chini ya ibara ya (1), mahakama inaweza kutoa amri au maelekezo yanayostahili- (a) kuzuia, kukomesha au kuachisha tendo au kosa lolote hatari kwa mazingira; (b) kumshurutisha afisa yeyote wa umma kuchukua hatua ya kuzuia au kukomesha tendo au kosa lolote hatari kwa mazingira; ama (c) kutoa fidia kwa mwathiriwa yeyote anayeathirika kutokana na ukiukaji wowote wa haki ya kupata mazingira safi na salama kiafya.

    Soma kifungu kamili →
  • Mlalamikaji hahitaji kuonyesha kwamba mtu amepata hasara au jeraha.
    Art. 70(3)

    (3) Kwa madhumuni ya Kifungu hiki, haitakuwa lazima kwa anayetoa maombi kuonyesha kwamba mtu amepata hasara au kujeruhiwa.

    Soma kifungu kamili →

Soma nakala halisi →

    Tafuta →