Sura 9, Sehemu 2 · Art. 138
Tararatibu katika uchaguzi wa Rais
- Mgombea huchaguliwa kuwa Rais kama akipata zaidi ya nusu ya kura zote na angalau asilimia 25 ya kura katika zaidi ya nusu ya kaunti.
Art. 138(4)
(4) Mgombea urais atatangazwa kuwa Rais iwapo atapokea- (a) zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi; na (b) angalau asilimia ishirini na tano ya kura zilizopigwa katika kila kaunti na kaunti ziwe zaidi ya nusu ya kaunti zote kwa jumla.
Soma kifungu kamili → - Kama hakuna mgombea anayeshinda, uchaguzi mpya hufanyika ndani ya siku 30 kati ya wagombea wawili wa juu.
Art. 138(5)
(5) Iwapo hakuna mgombeaji amechaguliwa, uchaguzi mwingine utafanyika upya katika kipindi cha siku thelathini baada ya uchaguzi uliopita, na katika uchaguzi huo mpya, wagombeji watakuwa- (a) mgombeaji au wagombeaji ambao walipata kura nyingi zaidi; na (b) mgombeaji au wagombeaji ambao walipata idadi ya pili ya wingi wa kura.
Soma kifungu kamili → - Mwenyekiti wa IEBC hutangaza matokeo ndani ya siku saba baada ya uchaguzi.
Art. 138(10)
(10) Katika muda wa siku saba baada uchaguzi wa urais, mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka- (a) atangaza matokeo ya uchaguzi; na (b) atawasilisha ripoti iliyoandikwa ya matokeo ya uchaguzi kwa Jaji Mkuu na Rais aliye mamlakani.
Soma kifungu kamili →
- Ili kushinda, mgombea lazima apate zaidi ya nusu ya kura zote na kuungwa mkono katika kaunti nyingi.
Art. 138(4)
(4) Mgombea urais atatangazwa kuwa Rais iwapo atapokea- (a) zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi; na (b) angalau asilimia ishirini na tano ya kura zilizopigwa katika kila kaunti na kaunti ziwe zaidi ya nusu ya kaunti zote kwa jumla.
Soma kifungu kamili →