Sura 10, Sehemu 1 · Art. 159
Mamlaka ya Mahakama
- Mamlaka ya mahakama yanatoka kwa wananchi na hutekelezwa na mahakama na mabaraza.
Art. 159(1)
(1) Mamlaka ya Mahakama yanatokana na watu, yanajikita katika mahakama na mahakama maalum zinazobuniwa kulingana na Katiba hii.
Soma kifungu kamili → - Kanuni ni pamoja na haki kwa wote bila kujali hali, haki kutochelewa, na kukuza njia mbadala za kutatua migogoro.
Art. 159(2)
(2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi ; (b) Haki haitacheleweshwa; (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3); (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa.
Soma kifungu kamili → - Njia za kitamaduni za kutatua migogoro hazipaswi kukiuka Mswada wa Haki au kuwa kinyume na haki na maadili.
Art. 159(3)
(3) Mbinu za kitamaduni za utatuaji wa migogoro hazitatumiwa kwa njia ambayo- (a) itakiuka Sheria za Haki; (b) itagongana na haki na maadili au kusababisha matokeo yatakayogongana na haki na maadili; (c) haiambatani na Katiba hii au sheria yoyote iliyoandikwa.
Soma kifungu kamili →
- Mahakama huamua kesi kwa haki, na kila mtu ni sawa mbele yao.