Sura 11, Sehemu 4 · Art. 188
Mipaka ya kaunti
- Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa azimio linalopendekezwa na tume huru na kupitishwa na Bunge la Kitaifa na Seneti, kila moja kwa angalau theluthi mbili.
Art. 188(1)
(1) Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa pendekezo tu- (a) lililopendekezwa na Tume huru iliyobuniwa na bunge kwa lengo hilo; na (b) iliyoidhinishwa na- (i) Baraza la Kitaifa likiungwa mkono na wabunge wasiopungua thuluthi mbili wa bunge hilo; na (b) seneti ikiungwa mkono na angalau wawakilishi wa kaunti wasiopungua thuluthi mbili ya ujumbe wa kaunti.
Soma kifungu kamili → - Mabadiliko huzingatia mambo kama idadi ya watu, miundombinu, uhusiano wa kihistoria na kitamaduni, na maoni ya jamii zinazohusika.
Art. 188(2)
(2) Mipaka ya kaunti inaweza kubadilishwa kwa kuzingatia- (a) wingi wa watu na uongezekaji wao; (b) miundomsingi na uhalisia wao; (c) mshikamano wa kihistoria na misingi ya kitamaduni; (d) gharama za usimamizi; (e) maoni ya jamii zilizoathirika; (f) malengo ya ugatuzi wa Serikali; na (g) sifa za kijiografia.
Soma kifungu kamili →
- Kubadilisha mipaka ya kaunti kunahitaji wingi mkubwa Bungeni na sababu nzuri.