Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 7 · Art. 194

Kuondoka afisini kama mwanachama wa baraza la kaunti

  • Ofisi ya mjumbe wa bunge la kaunti inakuwa wazi kama mjumbe akifa, akijiuzulu, akikosekana bila ruhusa, akiondolewa, au akikosa sifa.
    Art. 194(1)

    (1) Afisi ya mbunge wa baraza unge la kaunti huwa wazi kutokana na- (a) iwapo mbunge atafariki; (b) kama mbunge atakosa vikao vinane vya bunge bila idhini iliyoandikwa kwa spika wa bunge, na hawezi kutoa sababu za kutosha za kutohudhuria vikao hivyo; (c) kama mtu huyo ataondolewa afisini kwa mujibu wa Katiba hii au kwa mujibu wa sheria ya kifungu cha 80. (d) mbunge akijiuzulu kwa kumwandikia spika wa bunge; (e) iwapo baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge- (i) kama mwanachama wa chama cha kisiasa atajiuzulu, ama ikichukuliwa amejiuzulu kutoka kwa chama kwa mujibu wa sheria inayotajwa katika Ibara ya (2); au (ii) baada ya kuchaguliwa bungeni kama mgombea huru, anajiunga na chama cha kisiasa (f) kukamilika kwa kipindi cha bunge; au (g) kama mwanachama ataondolewa afisini kwa misingi ya uchaguzi ilivyowekwa katika Kifungu cha 193 (2).

    Soma kifungu kamili →
  • Kama mjumbe aliyechaguliwa kupitia chama akiacha chama hicho, kiti chake kinakuwa wazi.
    Art. 194(1)(e)(i)

    (i) kama mwanachama wa chama cha kisiasa atajiuzulu, ama ikichukuliwa amejiuzulu kutoka kwa chama kwa mujibu wa sheria inayotajwa katika Ibara ya (2); au

    Soma kifungu kamili →

Soma nakala halisi →

    Tafuta →