Sura 12, Sehemu 3 · Art. 211
Ukopaji wa Serikali ya Kitaifa
- Bunge linaweza kuweka masharti ambayo serikali ya kitaifa inaweza kukopa na kuweka mahitaji ya kuripoti.
Art. 211(1)
(1) Bunge kupitia kwa sheria, linaweza – (a) kueleza hali ambazo serikali ya kitaifa inaweza kukopa; na (b) kuweka kanuni za kutoa taarifa.
Soma kifungu kamili → - Katibu wa Baraza la Mawaziri anayeshughulikia fedha lazima awasilishe taarifa kuhusu mkopo au dhamana yoyote Baraza linapoomba.
Art. 211(2)
(2) Kati ya kipindi cha siku saba baada ya Bunge kutoa ombi, Waziri anayehusika na fedha atawasilisha habari kwa kamati husika kuhusu mkopo wowote au dhamana, pamoja na habari yote muhimu ili kuonyesha – (a) kiwango cha madeni yote ikiwa ni pamoja na mtaji na jumla ya faida inayodaiwa; (b) mkopo huo ulivyotumiwa au utakavyotumiwa; (c) Mikakati iliyopo ya kulipa mkopo huo; na (d) hatua zilizochukuliwa katika kulipa mkopo huo.
Soma kifungu kamili →
- Serikali ya kitaifa inapokopa, Bunge huweka kanuni na linaweza kudai maelezo.
Art. 211(1)
(1) Bunge kupitia kwa sheria, linaweza – (a) kueleza hali ambazo serikali ya kitaifa inaweza kukopa; na (b) kuweka kanuni za kutoa taarifa.
Soma kifungu kamili →