Art. 99
Sifa za kufaa na kutofaa katika kuchaguliwa kama Mbunge
- Ili kuwa mbunge, lazima uwe mpiga kura aliyejiandikisha na ukidhi masharti.
Art. 99(1)
(1) Isipokuwa wakati mtu amepigwa marufuku katika ugombeaji chini ya Ibara ya (2), mtu anaweza kuchaguliwa kama mbunge iwapo mtu huyo- (a) amesajiliwa kama mpigakura; (b) anaafiki kiwango chochote cha kielimu, kimaadili na ana uadilifu kama inavyoagizwa kwenye Katiba hii au na Sheria ya Bunge; na (c) ameteuliwa na chama cha kisiasa au mgombeaji wa kujitegemea anayedhaminiwa - (i) na angalau wapigakura elfu moja waliosajiliwa katika eneobunge katika uchaguzi wa Baraza la Kitaifa; na (ii) na angalau wapigakura elfu mbili waliosajiliwa katika kaunti kwa uchaguzi wa Seneti.
Soma kifungu kamili →