Art. 145
Kuondolewa kwa Rais kupitia kwa kura ya kutokuwa na imani
- Bunge linaweza kumwondoa Rais anayevunja sheria vibaya sana, kwa kufuata mchakato mkali.
Art. 145(1)
(1) Mwanachama wa Baraza la Kitaifa, iwapo ataungwa mkono na thuluthi moja ya Wabunge wote, anaweza kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Rais- (a) kwa misingi ya ukiukaji mkubwa wa Vifungu vya vya Katiba hii na na sheria nyingine yoyote. (b) ikiwa pana sababu kubwa za kuamini kwamba Rais amehusika katika uhalifu kulingana na sheria za kitaifa au kimataifa;au (c) utovu mkubwa wa nidhamu.
Soma kifungu kamili →