Art. 163
Mahakama ya Juu
- Mahakama ya Juu Zaidi ndiyo mahakama ya juu kabisa na huamua migogoro ya uchaguzi wa rais.
Art. 163(1)
(1) Kutabuniwa Mahakama ya Juu itakayojumuisha – (a) Jaji Mkuu, ambaye atakuwa rais wa mahakama hiyo; (b) Naibu Jaji Mkuu, ambaye – (i) atakuwa naibu wa Jaji Mkuu; na (ii) atakuwa Naibu wa rais wa mahakama hiyo; na (c) majaji wengine watano.
Soma kifungu kamili →