Art. 165
Mahakama Kuu
- Mahakama Kuu hushughulikia kesi nzito na masuala ya haki.
Art. 165(3)
(3) Kulingana na ibara ya (5), Mahakama Kuu ina – (a) mamlaka asilia yasiyokuwa na mpaka katika masuala ya uhalifu na masuala ya kiraia; (b) mamlaka ya kubaini iwapo haki au uhuru wa kimsingi katika Sheria ya Haki imenyimwa, kukiukwa, kuingiliwa au kutishiwa; au (c) mamlaka ya kusikiliza rufaa ya uamuzi wa mahakama maalum iliyoteuliwa chini ya Katiba hii kuchunguza kuondolewa kwa mtu kutoka afisini, tofauti na Tume iliyoteuliwa chini ya Kifungu cha 144; (d) mamlaka ya kusikiliza swala lolote kuhusu kufasiriwa kwa Katiba hii pamoja na kutoa uamuzi wa- (i) swali iwapo sheria yoyote inakiuka au kwenda kinyume na Katiba hii; (ii) swali iwapo chochote kinachosemwa kutekelezwa chini ya mamlaka ya Katiba hii au sheria yoyote, kinakiuka au kutekelezwa kinyume na Katiba hii; (iii) suala lolote linalohusu mamlaka ya kikatiba ya taasisi za serikali kwa mujibu wa serikali za kaunti na suala linalohusu uhusiano wa kikatiba kati ya viwango vya serikali; na (iv) swali linalohusu mkinzano wa sheria chini ya Kifungu cha 191.
Soma kifungu kamili →