Art. 174
Malengo ya ugatuzi
- Ugatuzi huleta serikali karibu na watu ili waweze kuamua kuhusu maeneo yao.
Art. 174(c)
Malengo ya Serikali ya ugatuzi ni- (a) kuhakikisha kuwa kuna mamlaka ya kidemokrasia na uwajibikiaji wa Serikali ; (b) kuhimiza umoja wa kitaifa kwa kutambua uanuwai wa jamii mbalimbali; (c) kuwapa watu katika kila ngazi mamlaka ya kujitawala na kushiriki katika matumizi ya mamlaka ya Serikali katika kufanya maamuzi ya mambo yanyowaathiri; (d) kutambua haki za jamii zote katika kusimamia masuala ya jamii zao na kujiendeleza zaidi; (e) kulinda na kuhamasisha maslahi na haki za jamii za watu walio wachache na zile za watu waliotengwa; (f) kustawisha miradi ya kijamii na kiuchumi na utoaji wa huduma za karibu na zilizo rahisi ili kumfikia kila mtu nchini Kenya; (g) kuhakikisha kuna ugavi sawa wa rasilmali zote za kijamii na za kitaifa kote nchini. (h) kufanikisha ugatuzi wa mamlaka ya taasisi za Serikali, uendeshaji wake wa shughuli ama huduma kutoka mji mkuu wa Kenya; na (i) kuhakikisha kuna kudhibiti na kugawana mamlaka kwa njia iliyo sawa.
Soma kifungu kamili →