Art. 230
Tume ya Mishahara na Kuzawidi
- Tume huamua kiasi cha malipo ya viongozi na maafisa wa umma.
Art. 230(1)
(1) Tume ya mishahara na kuzawidi inajumlisha watu wafuatao walioteuliwa na Rais – (a) Mwenyekiti (b) Watu walioteuliwa na mashirika yafutayo, ambayo watu ambao si wanachama au waajiriwa wa mashirika hayo wameteuliwa. (i) Tume ya Huduma za Bunge (ii) Tume ya Huduma za Umma (iii) Tume ya Huduma za Mahakama (iv) Tume ya Kuwaajiri Walimu (v) Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi (vi) Baraza la Ulinzi; na (vii) Seneti, kwa niaba ya serikali za kaunti; (c) Watu walioteuliwa, kila mmoja na – (i) Shirika kuu linalowakilisha vyama vya wafanyakazi; (ii) Shirika linalowakilisha waajiri; na (iii) Jopo la Muungano linaloshirikisha makundi ya wataalamu yaliyokubaliwa kisheria. (d) Watu walioteuliwa, kila mmoja na – (i) waziri anayesimamia fedha; (ii) Mwanasheria Mkuu; na (e) Mtu aliye na tajriba katika usimamizi wa wafanyakazi katika huduma ya umma, aliyeteuliwa na katibu wa Waziri anayesimamia huduma ya umma.
Soma kifungu kamili →