Art. 232
Maadili na Kanuni za Huduma za Umma
- Watendaji wa umma lazima wawe waaminifu, wa haki na kuwahudumia wote kwa usawa.
Art. 232(1)
(1) Maadili na Kanuni za Umma huhusisha– (a) viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma; (b) matumizi bora ya rasilmali; (c) utoaji wa haraka wa huduma za umma usio na upendeleo na unaozingatia usawa na haki; (d) ushirikishwaji wa watu katika utaratibu wa kuunda Sera; (e) uwajibikaji katika shughuli za kiusimamizi; (f) uwazi na utoaji wa habari sahihi kwa umma bila kuchelewa; (g) kwa kuzingatia ibara za (h) na (i), ustahili na ujuzi wa mtu ndio msingi wa kuteuliwa au kupandishwa cheo; (h) uwakilishi wa jamii mbalimbali za Kenya; na (i) kutoa nafasi sawa na za kutosha za kazi, katika kuteua, kutoa mafunzo na kupandishwa vyeo katika ngazi zote za huduma za umma, kwa- (i) wanaume na wanawake; (ii) watu wa jamii zote; na (iii) watu wenye ulemavu.
Soma kifungu kamili →