Sura 7, Sehemu 3 · Art. 91
Kanuni za kimsingi kwa vyama vya kisiasa
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kila chama cha kisiasa- (a) kitakuwa na sifa za kitaifa kama inavyopendekezwa na Sheria ya Bunge; (b) kiwe na taasisi ya kiutawala iliyochaguliwa kidemokrasia; (c) kitadumisha na kukuza umoja wa kitaifa; (d) kitazingatia kanuni za kidemokrasia za utawala bora, kudumisha na kuendeleza demokrasia kupitia kwa uchaguzi wa mara kwa mara, ulio na haki na huru katika chama; (e) kitaheshimu haki za kila mtu ili kushiriki katika harakati za kisiasa, yakiwemo makundi ya walio wachache na wale waliotengwa; (f) kitaheshimu na kudumisha haki za binadamu na uhuru wa kimsingi, na usawa wa kijinsia na usawazishaji; (g) kitadumisha malengo na kanuni za Katiba hii na utawala wa sheria; na (h) kitazingatia kanuni za maadili ya vyama vya kisiasa. (2) Chama cha kisiasa – (a) hakitabuniwa kwa misingi ya kidini, lugha, mbari, kabila, jinsia au kwa misingi ya kimaeneo au kujihusisha katika kampeni za kusambaza chuki na shihata katika misingi ya masuala mengine kama hayo; (b) hakitajihusisha na au kuchochea ghasia kwa, au vitisho kwa, wanachama wake, wafuasi, wapinzani au mtu mwingine yeyote; (c) hakitaanzisha au kufadhili vikosi vya jeshi la wanamgambo wa kuvizia, makundi haramu au mashirika mengine kama hayo; (d) hakitajihusisha katika utoaji hongo au aina nyingine za ufisadi; au (e) isipokuwa kwa jinsi ilivyoelezwa katika Sura hii au kwa mujibu wa Sheria ya Bunge, kukubali au kutumia rasilimali ya umma ili kuimarisha maslahi yake au wagombeaji wake katika uchaguzi.
Kwa maneno rahisi
- Kila chama cha siasa lazima kiwe na baraza linaloendeshwa kwa uchaguzi wa kidemokrasia.
Art. 91(1)(b)
(b) kiwe na taasisi ya kiutawala iliyochaguliwa kidemokrasia;
Soma kifungu kamili → - Vyama lazima vikuze umoja wa kitaifa na havipaswi kujikita katika misingi ya dini, rangi, kabila, jinsia au eneo.
Art. 91(2)(a)
(a) hakitabuniwa kwa misingi ya kidini, lugha, mbari, kabila, jinsia au kwa misingi ya kimaeneo au kujihusisha katika kampeni za kusambaza chuki na shihata katika misingi ya masuala mengine kama hayo;
Soma kifungu kamili → - Vyama havipaswi kujihusisha na vurugu, hongo au ufisadi.
Art. 91(2)(d)
(d) hakitajihusisha katika utoaji hongo au aina nyingine za ufisadi; au
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Vyama vya siasa lazima viwe vya haki, vya amani, na wazi kwa kila mtu.
Art. 91(1)(b)
(b) kiwe na taasisi ya kiutawala iliyochaguliwa kidemokrasia;
Soma kifungu kamili →