Sura 4, Sehemu 1 · Art. 24
Mipaka ya haki au uhuru wa kimsingi
- Haki inaweza kuwekewa mipaka kwa sheria tu, na tu pale mpaka huo unapokuwa wa haki na unastahili katika jamii huru na ya kidemokrasia.
Art. 24(1)
(1) Haki ya uhuru wa kimsingi iliyo katika Sheria ya Haki haiwezi kuwekewa mipaka isipokuwa kupitia kwa sheria na iwe tu kwamba mipaka ina maana, na ni ya haki katika jamii iliyo wazi na ya kidemokrasia, na chini ya misingi ya heshima ya binandamu, usawa na uhuru, na kwa kuzingatia vipengele muhimu vikiwemo- (a) hali ya haki hiyo au uhuru wa kimsingi; (b) umuhimu wa lengo la mipaka hiyo; (c) hali na kiwango cha mipaka hiyo; (d) haja ya kuhakikisha kuwa kufurahia wa haki hizo na uhuru huo wa kibinafsi kwa mtu yeyote hautatizi haki na uhuru wa kimsingi wa watu wengine; na (e) uhusiano uliopo kati ya mpaka na lengo lake na endapo kuna njia zingine zisizotatiza za kufikia lengo hilo.
Soma kifungu kamili → - Hata ukiwekewa mpaka, haki haiwezi kuondolewa maana yake ya msingi.
Art. 24(2)(c)
(c) halitazuia haki au uhuru wa kimsingi unaotajwa katika Sheria ya Haki ili kupunguza uzito na umuhimu uliowekwa katika haki hiyo.
Soma kifungu kamili → - Serikali lazima iweze kuonyesha mahakamani kwamba mpaka wowote wa haki unastahili.
Art. 24(3)
(3) Serikali au mtu anayetaka kuhalalisha mpaka fulani atapaswa kuthibitishia mahakama, mahakama maalum au mamlaka nyingine kuwa mahitaji ya Kifungu hiki yameridhishwa.
Soma kifungu kamili →
- Kanuni zingine zinaweza kuweka mpaka kwa haki, lakini tu kama ni za haki na zinahitajika kulinda wengine.