Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 7, Sehemu 1 · Art. 82

Sheria kuhusu uchaguzi

  • Bunge lazima litunge sheria kuhusu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi.
    Art. 82(1)

    (1) Bunge litatunga sheria ya kutoa nafasi ya- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuamua idadi ya maeneo-bunge kuhusu maeneo ya uchaguzi kwa wanachama wa Baraza la Kitaifa na mabaraza ya kaunti; (b) uteuzi wa wagombeaji; (c) usajili wa mara kwa mara wa raia kama wapiga kura; (d) hali ya chaguzi na kura za maamuzi. Uendeshaji na usimamizi bora wa chaguzi na kura za maamuzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombeaji wa uchaguzi; na (e) usajili wa mara kwa mara wa raia wanaoishi nje ya Kenya, kama wapiga kura na kuzifahamu haki zao za kupiga kura.

    Soma kifungu kamili →
  • Upigaji kura lazima uwe rahisi na wa wazi, na uzingatie watu wenye ulemavu na wengine wenye mahitaji maalum.
    Art. 82(2)

    (2) Sheria inayotakikana na ibara ya (1) (d) itahakikisha kwamba upigaji kura katika kila uchaguzi ni- (a) rahisi; (b) wazi; na (c) inazingatia mahitaji maalumu ya- (i) watu wenye ulemavu; na (ii) watu wengine ama vikundi vya watu walio na mahitaji maalumu.

    Soma kifungu kamili →

Soma nakala halisi →

    Tafuta →