Sura 8, Sehemu 4 · Art. 116
Kutekelezeka kwa sheria
- Sheria ya Bunge huchapishwa katika Gazeti ndani ya siku saba baada ya kuidhinishwa.
Art. 116(1)
(1) Mswada unaopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais, utachapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali kama Sheria ya Bunge katika muda wa siku saba baada ya kuidhinishwa; na
Soma kifungu kamili → - Sheria huanza kutumika siku ya kumi na nne baada ya kuchapishwa isipokuwa itataja tarehe nyingine.
Art. 116(2)
(2) Kwa kuzingatia ibara ya (3), Sheria ya Bunge inaanza kutekelezwa baada ya siku ya kumi na nne za kuchapishwa kwake katika Gazeti Rasmi la Serikali isipokuwa pale ambapo Sheria yenyewe inapendekeza tarehe au wakati wa kuanza kutekelezwa kwake.
Soma kifungu kamili →
- Baada ya Rais kusaini sheria, inatangazwa na kuanza kutumika karibu wiki mbili baadaye.